Wednesday, June 26, 2013

BARAFU JOGGING WAFANYA JOGGING PAMOJA NA WABUNGE MJINI DODOMA

Katika harakati za kuhamasisha mchezo wa mbio za pole pole (jogging) miongoni wa watunga sheria, klabu ya  Barafu Jogging ya Magomeni Dar es Salaam ilisafiri mpaka mkoani Dodoma na kufanya jogging pamoja na wabunge wa bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Miongoni mwa wabunge walioshiriki ni pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Hawa Ghasia, Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makalla, Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba,  Mbunge wa Kinondoni Idd Azan, Mbunge wa Nzega Dk. Khamis Kigwangala,  Mbunge wa Namtumbo, Vita Kawawa, n.k. Angalia picha za tukio hilo. Picha zote kwa hisani ya Shaffih Dauda Blog na Barafu Jogging
Mheshimiwa Iddi Azzan akiwaelekeza waheshimiwa wenzake namna ya kupanga mistari kwa ajili ya kukimbia jogging
Kutoka kushoto mbele kabisa ni waheshimiwa Iddi Azza, Amos Makala na Hawa Ghasia

Waheshimiwa wakikatiza mitaa ya Dodoma

Mara baada ya kukamilisha mbio za pole pole na kama ilivyo ada kwa wana-jogging washiriki wote walijumuika pamoja kwa ajili ya kufanya "aerobics" ambapo washiriki hufanya mazoezi kwa kumfuata kiongozi na midundo ya muziki.
Mheshimiwa Iddi Azzan akiwaongoza waheshimwa wenzake kujipanga kwa ajili ya "aerobics"

Waheshimiwa wabunge pamoja na wa Barafu Jogging wakifanya "aerobics" picha za chini pia wakiendelea na aerobics






 
Tunawapongeza sana wenzetu wa Barafu Jogging kwa kuhamasaisha mchezo wetu pendwa wa mbio za pole pole.

WANA-JOGGING WAJITOKEZA KWA WINGI KUMZIKA HELLEN MICHAEL ALIYEFARIKI KWA AJALI YA GARI ILIYOTOKEEA AKIWA KWENYE JOGGING

Jumapili ya tarehe 23 Juni, 2013 ilikuwa ni siku ya huzuni sana kwa wanamichezo hususani katika tasnia ya mbio za pole pole (jogging) kwa kumpoteza mwanachama wa klabu ya jogging ya Kopa - Mwananyamala Bi. Hellen Michael aliyefariki katika ajali ya gari ambayo ilitokea maeneo ya Viktoria, Barabara ya Mwai Kibaki, Kinondoni majira ya asubuhi. Ajali hiyo ambayo pia imeacha wanamichezo tisa wakiuguza majeraha huku wawili kati yao wakilazimika kufanyiwa upasuaji. Mwili wa marehemu uliwasili nyumbani majira ya saa 10:30 jioni na maziko yalifanyika saa 11 kasorobo jioni. Fuatilia matukio mbalimbali kwa picha.

Katibu Mkuu wa M'nyamala Jogging ambaye pia alikuwa ni mmoja wa waratibu wa shughuli za msiba akitoa taarifa mbalimbali za maandalizi ya mazishi

Katibu Mkuu wa Mzimuni Jogging Kabambura akitoa ufafanuzi wa jambo

Baadhi waombolezaji wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kunduchi Kwanza Asia Mohamed (Mwenye kofia) na Katibu wake Alphonsina Jospeh (mwenye mkoba)



Yahya Poli (katikati) Mratibu wa msiba akijadiliana jambo na Mwenyekiti wa Kunduchi Kwanza Asia Mohamed na Kocha Said wa Faita Jogging       
Jeneza lenye mwili wa marehemu Hellen Michael lilipowasili nyumbani kwa ajili ya mazishi
Mwili wa marehemu ukiswali tayari kwa ajili ya kuzikwa
Wana-jogging walipanga mstari kuanzia nyumbani mpaka makaburini

   




Diwani wa kata ya Mwananyamala Songoro Mnynge (mwenye suti) alikuwa ni sehemu ya waombolezaji
Kwa niaba ya uongozi wa Chama cha Jogging - Kinondoni, katibu Mkuu ndugu Yahya Poli anatoa pole tena kwa wafiwa na kuhimiza mshikamano miongoni mwa wana-jogging katika matukio kama haya. Tunamuombea pia marehemu Mwenyezi Mungu ampumzishe kwa amani.

Sunday, June 23, 2013

HABARI NA MATUKIO YA MAZOEZI YA PAMOJA KATI YA KUNDUCHI KWANZA NA BIAFRA LEO TAR 23 JUNI, 2013

Leo tarehe 23 Juni, 2013 wanamichezo toka klabu za Kunduchi Kwanza na Biafra walifanya mazoezi ya pamoja ya mbio za pole pole ambazo zilianzia katika viwanja vya Machava Kunduchi Mtongani na kuishia makao makuu ya klabu ya Kunduchi Kwanza yaliyopo Malanja Executive Inn Kuduchi Mtongani. Lengo la kufanya kufanya mazoezi ya pamoja lilikuwa ni kudumisha uhsuiano mwema uliopo baina ya klabu hizo mbili na pia kuwasilisha mchango wa Shilingi laki moja (100,000/=) ambazo wanabiafra waliahidi kama sehemu ya kuchangia gharama za ujenzi wa Makao Makuu ya klabu ya Kunduchi baada ya kupata ajali ya kuungua moto na kuteketeza ukumbi wa mikutano na sherehe. Fuatilia matukio katika picha.







Mara baada ya kureje klabuni, wanamichezo walifanya mazoezi ya kunyoosha viungo



Mara baada ya kunyoosha mwili wanamichezo wote walijumuika pamoja kwa ajili ya zoezi la kukabidhi mchango wa Biafra kwa Kunduchi Kwanza.

Mwenyekiti wa Biafra Akizungumza

Katibu Mkuu wa Biafra akizungumza

Katibu Mkuu wa Kunduhci Kwanza Alphonsina Joseph Mbusilo (aliyesimama) akiwashukuru wanabiafra

Mwenyekiti wa Biafra akimkabidhi mchango mweka hazina wa Kunduchi Kwanza


Friday, June 21, 2013

BIAFRA SPORTS CLUB NA KUNDUCHI KWANZA KUFANYA MAZOEZI YA JOGGING PAMOJA JUMAPILI TAR 23 JUNI, 2013

Katika kuimarisha uhusiano baina ya vilabu vya michezo hasa vinavyohamasisha mchezo wa mbio za pole pole (jogging), wanamichezo toka vilabu vya Biafra na Kunduchi Kwanza wameazimia kufanya mazoezi ya Jogging pamoja siku ya jumapili tarehe 23 Juni, 2013. Mazoezi hayo yataratibiwa na klabu ya Kunduchi Kwanza ambako ndiko yatapofanyikia . 
Michael Silili (mwenye vuvuzela) akihamasisha kwa wimbo
Wananchi na wakaazi wote wa maeneo ya kunduchi mnakaribishwa kujumuika pamoja katika jogging siku hiyo. 

Thursday, June 20, 2013

AROBAINI YA MOLLEL Jr. YAFANA

Wanabiafra pamoja na marafiki wengine kwa pamoja walijumuika nyumbani kwa Mwenyekiti wa Biafra Bw. Abdul Mollel pamoja na mkewe Bi. Evelyine katika arobaini ya mtoto wao Mollel Jr. Fuatilia matukio pichani.
Mama mzaa chema Evelyne akiwa na mtoto

Mollel na mkewe pamoja na mtoto wao

Mhamasishaji wa Biafra Chriss Matembo Mama Mollel Jr na Sada

Babuu Bwashee akimpongeza mama na mtoto

Emmy msechu naye akitoa pongezi

Kaka Poli akitoa pongezi

Wanabiafra

Wakati wa dua

#BYFT wakipata msosi

Biafra Queens wakipata msosi