Thursday, August 01, 2013

MCHEZO WA MBIO ZA POLE POLE (JOGGING) WAZIDI KUSHIKA KASI WILAYA YA KINONDONI

Kwa takriban miaka mitatu sasa watu wengi wamejikusanya pamoja na kuanzisha vilabu vya jogging katika manispaa ya kinondoni, mchezo ambao ni maarufu sana katika manispaa ya Temeke kwa mkoa wa Dar es Salaam ambapo ndipo yalipo maskani ya klabu kongwe ya mchezo huo ya Temeke Jogging. Klabu ambayo ni kongwe kwa manispaa ya Kinondoni ni Namanga Jogging ambayo ilianzishwa kwa zaidi ya miaka 8 iliyopita. 
Wana-jogging wakiwa mazoezi

Kwa mujibu wa utafiti mdogo uliofanywa na mwandishi wa habari hii, katika manispaa ya Kinondoni kuna vilabu zaidi ya 37 vya jogging katika kata mbalimbali na miongoni mwavyo, zaidi ya ya vilabu 15 tayari vimeshapata usajili rasmi katika Baraza la Michezo la Taifa ambayo ni mamlaka ya kisheria inayohusika na usajili wa vilabu na vyama vya michezo Tanzania.
Baadhi ya wana-jogging wa klabu ya Biafra katika picha ya pamoja
Klabu ya Michezo ya Biafra anyo iliyoanzishwa miaka takriban minne iliyopita nayo iliongeza hamasa zaidi ya kuanzishwa kwa vilabu vingine ambapo kila siku za mwisho wa wiki yaani jumamosi na jumapili barabara nyingi za manispaa hiyo hutumika na wana-jogging nyakati asubuhi. 


Wingi wa vilabu hivyo umepelekea haja ya kuhuisha Chama cha Jogging Kinondoni ambacho kilianzishwa kwa hamasa ya aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Kanali Fabian Massawe na kilipotea baada ya mkuu huyo wa wilaya kuhamishiwa katika wilaya nyingine.

No comments:

Post a Comment