Sunday, August 18, 2013

MAZOEZI YA JOGGING TARE 18 AGOSTI, 2013 YAZIKUTANISHA TENA BIAFRA NA NAMANGA

Katika kuimarisha mahusiano na ujirani mwema kwa vilabu vya jogging, wanamichezo kutoka vilabu vya Biafra na Namanga vilifanya mazoezi ya pamoja ambayo yalianzia mtaa wa Isere na kuingia barabara ya Kawawa hadi barabara ya kuelekea kwa Kopa mpaka kwenye makutano ya barabara ya Mwananyamala kuelekea Viktoria, kisha barabara ya Bagamoyo hadi Sayansi kwenye makutano ya barabara ya Rose Garden (Tembo Avenue) kutokea kwa Nyerere, kisha kufuata barabara ya Mwai Kibaki hado Moroko kuelekea Biafra na kumalizia klabuni. Fuatilia matukio kwa picha.
Tulikutana na vijana wa Mwendo Kasi Jogging (wenye jezi nyekundu)

Tulipata bahati ya kukutana na bibi ambaye alituunga mkono kwa kukimbia pamoja nasi







WOTE MNAKARIBISHWA KATIKA MAZOEZI YA MBIO ZA POLE POLE! 

MAZOEZI NI AFYA, ACHA KUJIACHIA!!!


Monday, August 12, 2013

HAFLA YA IFTAR YA WANABIAFRA KATIKA MATUKIO

Tarehe 8 Agosti, 2013 ambayo pia ilikuwa 30 Ramadhan, 1434 klabu ya michezo ya Biafra iliandaa hafla ya kushiriki pamoja katika iftar na kuuaga mwezi mtukufu wa Ramadhan. Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa Mheshimiwa diwani wa kata ya Mwananyamala ndugu Songoro Mnyonge pamoja na wageni waalikwa toka vilabu mbalimbali vinavyojihusisha mchezo wa mbio za pole pole (jogging), waandishi na watangazaji wa habari za michezo, wanablogu na wadau mbalimbali wa klabu ya Biafra.
Waheshimiwa Songoro Mnyonge (diwani wa mwananyamala) kulia na Faustine Makima M/Kiti serikali ya mtaa wa Balozi Msolomi/Isere

Mwenyekiti wa Kunduchi Kwanza Jogging Asia Mohamed (kulia)

Wanachama wa Kawe Social and Sports Club wakiwakilisha

Wawakilishi toka Kopa Generation Jogging

Watoto wa Biafra

Iftar ikiendelea






Watoto wa Biafra wakipata iftar

Wadau na mashabiki wa Biafra wakipata Iftar

Mhamasishaji na mwimbishaji wa Biafra Chriss akipata iftar

Katibu wa Biafra Kaka Poli akipata iftar


Mhamasishaji wa Biafra Kaka Hamza akipata Iftar

Katibu wa Kamati ya Ufundi ya Biafra Ally Juma akipata Iftar
Mheshimiwa Songoro Mnyonge - Diwani wa Mwananyamala akitoa neno la shukrani
Baada ya kumaliza hafla ya Iftar, mgeni rasmi katika hafla hiyo Mheshimiwa Diwani, Songoro Mnyonge  alipata wasaa wa kutoa neno la shukrani kwa Wanabiafra na pia kwa washiriki wote katika hafla hiyo ambapo pamoja na mambo mengine alieleza kufuruhaishwa sana tukio hilo na hivyo kumpa hamasa yeye ya kuona namna anavyoweza kushirikiana na klabu katika kuhamasisha michezo na maendeleo miongoni mwa wanajamii. Pia alitumia fursa hiyo kuelezea kinagaubaga nia yake ya kuwa mwanachama wa klabu ya michezo ya Biafra. Wanabiafra walipokea maombi ya mheshimiwa Diwani kwa shangwe na faraja na kumkaribisha rasmi katika klabu yao.
Katibu wa Biafra akiagana na wageni mheshimiwa Diwani (katikati) na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa
Klabu ya michezo ya Biafra inatoa shukrani za dhati kwa wadau wote waliofanikiwa kushiriki moja kwa moja katika hafla ya Iftar wakiwemo marafiki kutoka vilabu mbalimbali. Tumefurahi kujumuika pamoja, karibuni sana!

Thursday, August 01, 2013

BELLE 9, YOUNG KILLER, BRIGHT NA WASANII KIBAO KUTUMBUIZA KATIKA MIJI YA MBEYA NA TUNDUMA SIKUU YA IDD MOSI NA IDD PILI

Katika kuwasogezea burudani karibu kabisa, kampuni ya Robik General Supplies Ltd imeandaa maonyesho ya muziki kwa wakazi wa miji ya Mbeya, Tunduma na maeneo ya jirani katika kusherehekea sikuu ya Idd mosi na Idd pili. Akizungumza na mwandishi wetu, mkurugenzi wa Robik ndugu Robert Mwakibugi alieleza kwamba sikukuu ya Idd mosi na Idd pili burudani itatolewa na wasanii Belle 9 Young Killer, Bright na wengineo ambapo Idd mosi onyesho litafanyika katika ukumbi wa Honeymoon Hotel mjini Tunduma na Idd pili onesho litafanyika katika ukumbi wa Mtenda Sunset Hotel Mbeya mjini. 

Mratibu wa matukio wa kampuni hiyo ndugu Boniface Harrison amebainisha kwamba kila kitu kinakwenda vizuri na tayari wasanii wote wamethibitisha kushiriki katika maonesho hayo ambayo yanadhaminiwa na Mtenda Sunset Hotel & Conference Centre, Honeymoon Hotel pamoja na Chimbinga Unique Pub. Pia alitoa fursa kwa wadhamini wengine kujitokeza kudhamini maonesho hayo.  

MCHEZO WA MBIO ZA POLE POLE (JOGGING) WAZIDI KUSHIKA KASI WILAYA YA KINONDONI

Kwa takriban miaka mitatu sasa watu wengi wamejikusanya pamoja na kuanzisha vilabu vya jogging katika manispaa ya kinondoni, mchezo ambao ni maarufu sana katika manispaa ya Temeke kwa mkoa wa Dar es Salaam ambapo ndipo yalipo maskani ya klabu kongwe ya mchezo huo ya Temeke Jogging. Klabu ambayo ni kongwe kwa manispaa ya Kinondoni ni Namanga Jogging ambayo ilianzishwa kwa zaidi ya miaka 8 iliyopita. 
Wana-jogging wakiwa mazoezi

Kwa mujibu wa utafiti mdogo uliofanywa na mwandishi wa habari hii, katika manispaa ya Kinondoni kuna vilabu zaidi ya 37 vya jogging katika kata mbalimbali na miongoni mwavyo, zaidi ya ya vilabu 15 tayari vimeshapata usajili rasmi katika Baraza la Michezo la Taifa ambayo ni mamlaka ya kisheria inayohusika na usajili wa vilabu na vyama vya michezo Tanzania.
Baadhi ya wana-jogging wa klabu ya Biafra katika picha ya pamoja
Klabu ya Michezo ya Biafra anyo iliyoanzishwa miaka takriban minne iliyopita nayo iliongeza hamasa zaidi ya kuanzishwa kwa vilabu vingine ambapo kila siku za mwisho wa wiki yaani jumamosi na jumapili barabara nyingi za manispaa hiyo hutumika na wana-jogging nyakati asubuhi. 


Wingi wa vilabu hivyo umepelekea haja ya kuhuisha Chama cha Jogging Kinondoni ambacho kilianzishwa kwa hamasa ya aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Kanali Fabian Massawe na kilipotea baada ya mkuu huyo wa wilaya kuhamishiwa katika wilaya nyingine.

Tuesday, July 30, 2013

MWANANYAMALA JOGGING KUFANYA UCHAGUZI MKUU TAREHE 25 AGOSTI, 2013

Katika pita pita ya mwandishi wa blogu hii ya Biafra kwenye magazeti ya Jumanne tarehe 30 Julai, 2013, amekutana na habari ya njema kuhusu uchaguzi wa mkuuwa viongozi wa klabu ya Mwnanyamala Jogging. Kwa mujibu wa mwandishi wa gazeti hilo la Tanzania Daima Bi. Elizabeth John, uchaguzi huo umepangwa kufanyika tarehe 25 Agosti, 2013 ambapo kabla ya uchaguzi huo zoezi la uchukuaji fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi linatarajiwa kufungwa tarehe 3 Agosti na usaili unatarajiwa kufanyika tarehe 8 Agosti, 2013.
Habari yenyewe ndio hii

Ally Salum "Chisco" Katibu Mkuu wa muda wa mwananyamala Jogging
Biafra Sports Club inawatakia mwananyamala Jogging Uchaguzi huru na wa haki.