Jumamosi iliyopita tarehe 29 Oktoba, 2012 mtoto wa Kinondoni Msisiri ambaye kwa sasa anauwakilisha vyema mkoa wa Morogoro Francis Cheka alizidi kuonesha ubabe kwa mabondia wenzake hasa wa Tanzania baada ya kumtandika kwa TKO katika raundi ya sita mwanamasumbwi mwenye makeke na maneno mengi Kalama Nyilawila. Mpambano huo uliopigwa katika ukumbi wa PTA Sabasaba ulishuhudiwa na mamia ya mashabiki wa mchezo wa ngumi huku mgeni rasmi akiwa ni Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Afande Suleiman Kova.
|
Bondia Francis Cheka akipima uzito |
|
Bondia Kalama Nyilawila akipima uzito |
Mpambano huo ulikuwa ni wa kuwania ubingwa wa mabara wa UBO mkanda ambao ulikuwa wazi ulizidi kumweka katika nafasi nzuri ya mchezo wa ngumi duniani Francis Cheka ambaye ni bingwa wa ngumi za kulipwa anayetambuliwa na vyama vya ICB, IBF na WBC na sasa UBO.
|
Bondia
Karama Nyilawila kulia akijitahidi kukwepa makonde ya Francis Cheka |
|
Bondia Francis Cheka (kulia) akimsukumia konde Kalama Nyilawila |
Katika raundi tano za kwanza Nyilawila alionyesha kumdhibiti kiasi Cheka kwa kumchezea
'kibabebabe' huku akitumia nguvu nyingi kujihami hali iliyopelekea baadhi ya mashabiki wa Nyilawila kushangilia kwa nguvu huku wa kuwa mwisho wa tambo za Cheka ulikuwa umewadia.
Hata hivyo raundi ya sita ilipoanza Cheka alionyesha amebadilika na hasa
baada ya kocha wake Abdallah Saleh 'Komando' kupanda ulingoni na
kuzungumza na bondia huyo na kumshushia kipigo Nyilawila, ambapo moja ya
makonde matatu ya mfululizo yalimpeleka chini mpinzani wake ambapo mwamuzi wa pambano hilo, Jerome Waluza alimhesabia Nyilawila ambaye
alijitahidi kuinuka, lakini ghafla akaonyesha ishara kwamba asingeweza
kuendelea na pambano hilo.
Baada ya kuonyesha ishara hiyo, mashabiki wa Cheka walilipuka kwa shangwe kkushangilia ushindi huo wa TKO. Itakumbukwa kuwa hii ni mara ya ili kwa Cheka kumpiga Nyilawila
|
Mgeni rasmi Kamanda Kova (kulia) akimnyanyua mkono Francis Cheka kuashiria ushindi |
Klabu ya Michezo ya Biafra inampa pongezi nyingi Bondia Francis Cheka (mtoto wa nyumbani) kwa ushindi huo.