Friday, September 28, 2012

KLABU YA MICHEZO YA BIAFRA YAJIPANGA KUWAKABIDHI RASMI BARUA ZA UTEUZI VIONGOZI WAKE JUMAPILI TAREHE 30 SEPTEMBA, 2012

Mwenyekiti mteule wa Klabu ya Michezo ya Biafra Bw. Abdul Mollel anawakaribisha wanachama, mashabiki pamoja na wadau wote kwa ujumla katika hafla ya kukabidhi barua za uteuzi kwa viongozi wote waliochaguliwa katika uchaguzi uliofanyika tarehe 16 Septemba, 2012. Hafla hiyo itafuatiwa na mazoezi ya pamoja ya mbio za polepole zitakazofanyika kuanzia majira ya saa 12:15 asubuhi makao makuu ya klabu 90 Degrees Pub Kinondoni na kuishia hapo hapo klabuni. 
Mwenyekiti mteule wa Biafra Abdul A. Mollel akitoa shukrani kwa wasimamizi wa uchaguzi, wanachama na wadau wote kwa kuweza kufanikisha uchaguzi huo.
Akielezea mazoezi ya mbio za pole pole (jogging) siku hiyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya Klabu Mr. Michael Silili alibainisha kwamba mazoezi yataanzia klabuni saa 12:15 asubuhi na kupitia barabara ya Kawawa na kuvuka Moroko kisha barabara ya migombani mpaka hospitali ya Mikocheni hadi viktoria na kukatisha baraba ya kuelekea mwananyamala kisha kupitia barabara ya kwakopa hadi kanisani na kumalizia klabuni kupitia barabara ya Isere.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi Michael Silili (Kulia) akiwa na mjumbe wa kamati hiyo Nancy Rafael wakifuatilia jambo kwa makini.

Akimalizia, Katibu Mkuu Mteule Bw. Yahya Poli aliwakaribisha wadau wote hata wale ambao si wanachama kwa mazoezi ya pamoja na baadaue hafla hiyo ya kukabidhi rasmi barua za uteuzi kwa viongozi wa klabu. Kwa wale ambao wanapenda kushiriki basi wanaweza kuwasiliana na katibu huyo kwa namba ya 0715253653.

 WE! WE! MAZOEZI NI AFYA, ACHA KUJIACHIA!

Tuesday, September 25, 2012

BIAFRA YOUTH FOOTBALL TEAM INAKUOMBA UCHANGIA VIFAA VYA MICHEZO ILI KUENDELEZA VIPAJI VYA SOKA KWA VIJANA

Timu ya vijana ya Biafra inawaomba wadau wote wa michezo uwezeshwaji wa vifaa vya michezo kwa ajili ya kuimarisha vipaji vyao na kulisaidia taifa kwa siku za usoni. Akizungumza baada ya mazoezi ya timu yao katika viwanja vya Biafra Kinondoni nahodha hiyo Hussein Tahidin (pichani chini) alisema timu yao zaidi ya kucheza mpira na kukuza vipaji vyao lakini pia wanapata fursa ya kuwa pamoja kama marafiki na kujiondoa kwenye vishawishi mbalimbali na tabia zisizofaa kwenye jamii. 
Hussein Tahiddin - Nahodha
 Wakibainisha mahitaji yao, nahodha huyo pamoja na wachezaji wenzake wameeleza kwa masikitiko kuwa wanahitaji mipira, jezi, viatu, soksi, koni za mazoezi, nyavu za magoli pamoja na vifaa vingine vya michezo kwa kadri wadau watakavyoona vinafaa kwa wachezaji hao. 




Pia kwa kupitia uongozi wa klabu yao ya Biafra Sports Club vijana hao wanaomba udhamini wa timu yao ili waweze kushiriki mashindano mbalimbali ili waweze kupima uwezo wao.

MDAU! KAMA UMEGUSWA NA MAOMBI YA VIJANA HAWA NA UNGEPENDA KUWASAIDIA, UNAWEZA KUWASILIANA NA KATIBU MKUU WA BIAFRA SPORTS CLUB KWA SIMU +255 715 253 653, BARUA PEPE: biafra.jsclub@gmail.com

MISAADA YOTE ITAKAYOTOLEWA ITATANGAZWA HAPA!

Monday, September 24, 2012

TANZIA TANZIA TANZIA TANZIA

Klabu ya Michezo ya Biafra pamoja na wadau wake wote wanaungana kwa pamoja katika msiba wa mama mdogo wa mwanachama wake Bi. Betty Mdeka ambaye ni mjumbe katika kamati ya Uchumi, Mipango na Fedha ya Klabu.Shughuli za mazishi zinafanyika nyumbani kwa marehemu maeneo ya Sinza Legho na maziko yatafanyika katika makaburi ya Kinondoni tarehe 24 Septemba, 2012.
Bi Happy Mdeka kushoto akiwa na mwanachama wa namanga jogging

Kwa pamoja tunamuomba mwenyezi mungu amtie nguvu mwanachama mwenzetu na pia mwenyezi mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi amen!

Monday, September 17, 2012

BIAFRA YAFANYA UCHAGUZI WA VIONGOZI KWA MAFANIKIO

Jumapili ya tarehe 16 Septemba 2012 ilikuwa ni siku ya uchaguzi wa viongozi wa klabu. Uchaguzi huo ulifanyika chini ya usimamizi wa viongozi wa michezo wilaya ya Kinondoni. Kufanikiwa kwa uchaguzi huo ambao ulifanyika katika makao makuu ya klabu, 90 Degrees Pub Kinondoni kulitokana na hamasa ya wanachama kujitolea katika kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kama zilivyobainishwa katika katiba ya klabu. 
BAADHI YA WANABIAFRA WAKIWA KLABUNI KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU SEPTEMBA 16, 2012          

Wagombea wa nafasi mbalimbali wakisubiri kuanza kwa zoezi la uchaguzi kutoka kushoto ni Ibrahim Kilasa, Freddy Mwesigwa (wagombea nafasi ya Kamati ya Uchumi na Mipango), na Abdul Mollel (mgombea nafasi ya Mwenyekiti)



Bi. Jacqueline Barozi (mgombea nafasi ya Makamu M/Kiti) akiwa na Mustafa Muro (mgombea Kamati ya Nidhamu na Rufaa




Nancy Raphael (mgombea kamati ya Ufundi) katikati akiwa na wagombea wenza Mossi Saidi (kushoto) na Boniface Banga (kulia)
 UCHAGUZI huo pia ulihudhuriwa na klabu rafiki za Namanga na Kunduchi kwanza ambapo wanachama toka klabu hizo walijumuika kwa pamoja na Wanabiafra katika kuhakikisha zoezi hilo la uchaguzi linafanikiwa. Wakiongozwa na Mwenyekiti wao Bi. Asia Mohamed, Wanakunduchi Kwanza waliwasili katika makao maku ya klabu ya Biafra majira ya saa nne asubuhi na muda mfupi baadae wanachama wa Namanga Sports Club nao waliwasili eneo hilo.
Mwenyekiti wa Kunchi Kwanza Jogging (wa kwanza kushoto) akiteta jambo na baadhi ya Wanakunduchi Kwanza


John Gako kutoka Namanga akiomba utaratibu toka kwa 'floor manager' wa shughuli Bi. Magreth Warisanga (aliyesimama)
VIONGOZI kutoka idara ya Michezo Manispaa ya Kinondoni waliwasili ukumbini hapo majira ya saa sita mchana na mara baada ya kupokelewa na kutoa salam zao za uchaguzi, moja kwa moja walitoa mwongozo wa namna zoezi zima la uchaguzi litakavyofanyika baada ya kuridhika na maandalizi ya uchaguzi wenyewe. 
Mr. Mrimi kutoka idara ya Michezo Manispaa ya Kinondoni (Katikati) akiteta jambo na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Balozi Msolomi, Isere, Mwinyimadi Tambaza (kushoto) msimamizi wa soka kwa watoto wadogo KIDYOSA

Wasimamizi wa uchaguzi wakifuatalia kwa makini maelezo ya mgombea (haonekani pichani)
MARA baada ya kukamilika kwa zoezi la kujieleza, wanachama walianza moja kwa moja zoezi la upigaji kura ambapo baada ya kukamilika kwa zoezi hilo wagombea wa nafasi za juu za klabu walipendekeza mawakala wao katika zoezi la kuhesabu kura.
Mawakala wa wagombea pamoja na wasimamizi wa uchaguzi wakiwa katika zoezi la kuhesabu kura

Zoezi la kuhesabu kura likiendelea

zoezi la kuhesabu kura likiendelea

Wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti na Makamu wake pamoja na wagombea wengine wakisubiri kwa hamu matokeo ya uchaguzi

Wagombea wa nafasi ya Kamati ya Ufundi wakisikiliza matokeo ya uchaguzi kwa hamu
ZOEZI la kuhesabu kura ambalo lilidumu kwa takriban masaa mawili lilikamilika na hatimaye msimamizi mkuu wa uchaguzi pamoja na jopo lake walirejea katika ukumbi wa mkutano na moja kwa moja kuanza kutangaza matokeo ya uchaguzi kwa kuanzia na wateule wa kamati za Ufundi, Uchumi na Mipango, Nidhamu na Rufaa na kisha Kamati ya utendaji, Mweka Hazina, Katibu Msaidizi, Katibu Mkuu, Makamau Mwenyekiti pamoja na Mwenyekiti. 
WASHINDI - KAMATI YA UCHUMI NA MIPANGO

AKIPONGEZWA KWA USHINDI WA NAFASI YA MWENYEKITI NDUGU ABDUL MOLLEL (KATIKATI)

WASHINDI WA NAFASI MBALIMBALI WAKIONGOZWA NA VIONGOZI WAKUU

MWENYEKITI MTEULE WA BIAFRA SPORTS CLUB, ABDUL MOLLEL AKITOA SHUKRANI KWA NIABA YA VIONGOZI WATEULE KWA WANACHAMA, WADAU NA MASHABIKI KWA KUFANIKISHA ZOEZI LA UCHAGUZI

MAKAMU MWENYEKITI MTEULE AKITETA JAMBO NA KATIBU MKUU MTEULE

MWINYIMADI TAMBAZA AKSISITIZA UMUHIMU WA KUIENZI TIMU YA WATOTO WA BIFRA KIDS

SHUGHULI ya uchaguzi ilikamilika majira ya saa moja jioni ambapo washindi pamoja na wanachama na wadau wengine wote walijumuika kwa burudani mbalimbali zilizotolewa ili kukamilisha siku hiyo maalum.

TUNAWAPONGEZA SANA VIONGOZI WOTE WALIOSHINDA PAMOJA NA WANACHAMA WOTE WA BIAFRA SPORTS CLUB, USHINDI WENU UWE CHACHU YA KULETA MAENDELEO YA KLABU NA MICHEZO KWA UJUMLA!