Tuesday, January 31, 2012

MATUKIO YA KUKUMBUKWA YALIYOFANYWA MWAKA 2011 NA KLABU YA MICHEZO YA BIAFRA

Mwaka 2011 ni mwaka wa kukumbukwa sana kwa klabu ya michezo ya Biafra. Mwaka huo kwa ushirikiano wa dhati na upendo wa hali ya juu kati ya wanachama, mashabiki, wapenzi wa klabu, wadau pamoja na jamii kwa ujumla.

Tukio la kwanza kubwa kabisa lilikuwa ni la uzinduzi wa klabu ambalo lilifanyika katika viwanja vya Biafra kwa shughuli mbalimbali za kimichezo na kuishia katika makao makuu ya klabu 90 Degrees Pub, Mtaa wa Isele Kinondoni kwa burudani mbalimbali.

Katika kusherehekea sikukuu sikuu ya Iddi Mosi mwezi Agosti, 2011 klabu ilifanikiwa kuandaa tamasha la michezo lililoambatana na hafla ya chakula cha mchana pamoja na burudani mbalimbali kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu toka katika vituo vya OneStop, Hanasif, Boko, n.k. Siku hiyo michezo mbalimbali kama vile mbio fupi, kuvuta kamba, kukimbiza kuku, mpira wa miguu, mchezo wa rede ilifanyika katika viwanja vya Biafra iliyofuatiwa na mashindano ya kuimba, chemsha bongo, kucheza muziki n.k. vilifanyika katika ukumbi wa klabu pale 90 Degree Pub.

 Mkurugenzi wa Biafra Sports Club Asha Warisanga (mwenye fulana nyekundu) akiimbisha nyimbo wakati wa mbio za pole pole


 Baadhi ya wageni kutoka mataifa mbalimbali walioshiriki tamasha la watoto yatima wakishiriki katika mbio za pole pole pamoja na wanabiafra

 Sehemu ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu walioshiriki mbio za pole pole

Watoto wakishindina mbio za mita 100 katika viwanja vya Biafra

Wanabiafra Jacqueline Barozi (kushoto) na Emeldah Mwakangale (kulia)  

 Mwenyekiti wa Serikali ya taa wa Balozi Msolomi Mzee Faustin Makima (mwenye kofia) akiiwakilisha vyema Biafra katika mbio za pole pole

Kikosi cha Biafra Kids a.k.a The Juniors ambacho kiliumana na kombaini ya timu ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu


Mshindi wa kukimbiza akipongezwa

Watoto wakisoma risala mara baada ya kurejea klabuni  toka tamashani


 Baadhi ya watoto kutoka katika kituo cha Hanasif Orphanage Centre wakifuatilia matukio mbalimbali yaliyokuwa yakiendelea

 Sehemu ya watoto wakiiwakilisha Biafra pamoja na watoto wenzao kutoka vituo vya kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu

 Miongoni mwa watoto waliomba vizuri na kukonga nyoyo za watu

Mwenyekiti wa Namanga Sports Club David Mwaka akikabidhi zawadi ya fedha kwa mkurugenzi wa Biafra Sports Club ambaye alipokea kwa niaba ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu toka vituo mbalimbali

Mara baada ya kufanikisha tamasha la michezo na hafla ya chakula cha mchana kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu, klabu iliendelea na mchakato wake wa kuandaa katiba yake ambapo hadi kukamilika kwa mchakato huo, vikao vitatu vilifanyika. Kikao cha kwanza cha katiba kilifanyika tarehe 4 Septemba, cha pili kilifanyika  tarehe 11 Septemba, 2011 na cha mwisho kilifanyika tarehe 18 Septemba, 2011 ambapo hatimaye katika kikao hicho ikapitishwa katiba ya Biafra Sports Club ambayo ilikuwa na ridhaa ya wanachama wote wa klabu. Hadi mchakato huo wa kuandaa katiba unakamilika, shukrani za dhati pia ziwafikie viongozi na wanachama kutoka katika klabu rafiki za Namanga na Kunduchi Kwanza kwa michango yao adhimu.
 Baadhi ya wanachama wa Biafra wakichambua baadhi ya katiba zilizowasilishwa
Robert Mwakibugi (mwenye fulana nyeupe) akisikiliza hoja mbalimbali zilizokuwa zikitolewa

 Mwenyekiti wa Kunduchi Kwanza Bi. Asia Mohamed akiwa pamoja na mweka hazina wa namanga Michael Juma a.k.a. Mopao wakifuatilia kwa makini kikao cha katiba

Ili kutoa fursa kwa kila mshiriki kuona kilichokuwa kikiandikwa katika kuandaa katiba ya klabu zilitumika teknolojia mbalimbali kama inavyoonekana pichani

Mara baada ya kukamilika kwa zoezi la uandaaji/uandishi wa katiba ya klabu  kukamilika pamoja na mambo mengine, wanachama waliamua kwa pamoja kubadilisha jina la klabu toka Biafra Jogging and Sports Club na kuwa "Biafra Sports Club" ambapo moja ya malengo yake ni kujihusisha na michezo mbalimbali na kwa kuanzia ni kuwa na timu ya watoto ya mchezo wa Soka ambayo itaitwa "Biafra Kids a.k.a. The Juniors".

Katika kuadhimisha miaka 50 ya uhuru, klabu ilidhamiria kuendelea kujitolea kwa jamii kama ambavyo imekuwa ikifanya katika matukio kadhaa yaliyopita. Klabu ilijipanga kufanya usafi wa mazingira pamoja na kutoa msaada kwa wagonjwa katika hospitali ya Mwananyamala ambayo ni hospitali ya wilaya ya Kinondoni. Baada ya kuwasilisha nia hiyo kwa klabu rafiki za Namanga na Kunduchi, ilionekana ni vyema tukaungana kwa pamoja katika kulifanikisha jambo hilo ndipo ilipoundwa kamati maalum iliyojumuisha wajumbe toka katika klabu zote tatu. Hatimaye kamati kwa kushirikiana na wanachama toka klabu zote tatu, marafiki na wadau mbalimbali wa michezo ilifanikisha zoezi hilo kama lilivyopangwa  tena kwa kupitiliza malengo yake.

 Mustafa Muro wa Biafara akipumzika baada ya mbio za pole za kuchangisha pesa kwa ajili ya kufanikisha zoezi la kufanya usafi wa mazingira hospitalini hapo na kutoa msaada kwa wagonjwa, shughuli hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Royal Billy's Lodge Tegeta Tangi Bovu

 Baadhi ya wanamichezo wakifanya 'aerobics' iliyokuwa ikongozwa na Michael Juma a.k.a Mopao

 Kutoka kushoto ni Asha M. Warisanga Mkurugenzi wa Biafra, Tobias Owur Mkurugenzi wa Royal Billy's Lodge na Abdul Mollel Mwenyekiti wa Biafra Sports Club

Kutoka kulia Ally S. Masharubu, Yahya Poli a.k.a Kaka Poli Katibu wa Biafra na Jacqueline Barozi wakiiwakilisha vyema Biafra


 Henry Maseko wa Biafra

Mwenyekiti wa Namanga Sports Club David Mwaka akiendesha harambee

 Charles Juma wa Namanga pamoja na Kaka Poli wa Biafra wakishirikiana kuweka hesabu vizuri katika harambee

 Njia mbalimbali za ubunifu katika kuongeza michango zilitumika kama hii ambapo Charles Juma alipewa adhabu na ili kumkomboa asitumikie adhabu hiyo ilibidi wadau walipie pesa

 Mwenyekiti wa kamati ya ufanikishaji wa shughuli hiyo Abdul Mollel akihesabu fedha taslimu zilizochangwa kwenye harambee



 Ilipowadia tarehe 9 Disemba, 2011 wanamichezo walijumuika pamoja katika viawanja vya biafra na kuanza mbio za pole pole kuelekea katika hospitali ya Mwananyamala


 Mwenyekiti wa kamati ya Habari John Badi akiwa na kitendea kazi tayari kupiga picha matukio yaliyokuwa yakiendelea hospitalini hapo
 Baadhi ya viongozi klabu mbalimbali wakikabidhi msaada wa biskuti kwa uongozi wa hospitali

 Akiiwakilisha vyema klabu ya Kunduchi Kwanza dada Sizya (mwenye nguo nyekundu) akifanya usafi eneo la mapokezi katika hospitali ya Mwananyamala

 Mwimbishaji wa klabu ya Biafra Michaele Silili akimjulia hali mgonjwa katika wodi ya wanaume hospitali ya Mwananyamala


 Mwanakamati Ibrahim Lincoln akiokota takataka




 Makamu Mwenyekiti wa namanga akipokea cheti cha kutambua mchango wa klabu yake katika kufanikisha zoezi zima


 Wengine walifanya usafi huku wakijiburudisha kwa nyimbo na kucheza

Mweka Hazina wa klabu ya Namanga Michael Juma akimkabidhi kopo la maziwa ya cowbell mama aliyetoka kujifungua hospitalini

Zoezi la kufanya usafi wa mazingira  pamoja na kugawa misaada kwa wagonjwa katika hospitali ya Mwananyamala lilifanikiwa kutokana na ushirikiano mkubwa ulioonyeshwa na wadau mbalimbali wakiwemo wale waliotoa vitu moja kwa moja kama vile kampuni ya Esoshi General Trading waliotoa pakiti zaidi ya mia nne za maziwa ya Tanga Fresh, kampuni ya TKT waliotoa chupa zaidi ya 90 za maji ya uhai, Royal Billy's Lodge waliochangia fedha taslim pamoja na fulana 60, Klabu za Namanga, Kunchi Kwanza pamoja na Biafra ambazo kila klabu ilichangia fedha taslimu shilingi laki moja na 90 Degrees Pub.


Kwa mara nyingine tena wanabiafra walipata fursa ya kujumuika pamoja na kula chakula cha jioni pamoja na kucheza muziki katika kusherehekea sikukuu ya krismasi ambapo wanachama walijumuika pamoja na marafiki na familia zao.

Hayo ni baadhi tu ya mambo ambayo klabu yako uipendayo ya Biafra imeyatekeleza kwa mwaka 2011. Karibu ujiunge nasi katika kuendelea michezo, hasa mchezo wa mbio za pole pole (jogging) pamoja na kuleta maendeleo kwa klabu, wanachama na jamii kwa ujumla katika mwaka 2012 na kuendelea.



 

Monday, January 30, 2012

AROBAINI YA MAREHEMU HASSAN kUKURU YAPANGWA KUFANYIKA TAREHE 5 FEBRUARI, 2012

Kwa wanachama, mashabiki, wapenzi na wadau wote wa klabu ya michezo ya Biafra, kwa niaba ya mwanabiafra mwenzetu Chande Kukuru, napenda kuchukua fursa hii kuwakumbusha kuwa arobaini ya marehemu Hassan Kukuru aliyefariki tarehe 25 Disemba, 2011 kwa ajali ya gari na hatimaye kuzikwa nyumbani kwao Bunju nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam tarehe 26 Disemba, 2011 itafanyika Jumamosi tarehe 5 Februari, 2012 Kinondoni.


Mwanabiafra Chande Kukuru (mwenye shati jeusi lenye mistari meupe) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na wanachama wa Biafra Sports Club mara baada ya mazishi huko Bunju.


Wanabiafra wote kwa ujumla wetu tunakumbushwa kumalizia michango yetu ya rambirambi na pia kushiriki kikamilifu katika kukamilisha arobaini ya marehemu Hassan Kukuru.

 Baadhi ya wanabiafra waliohudhuria ibada ya mazishi ya marehemu Hassan Kukuru iliyofanyikakatika msikiti wa Taqwa kabla ya kusafirishwa kwenda Bunju kwa mazishi wakiongozwa na mwenyekiti wa Biafra Sport Club (wa pili kutoka kushoto waliokaa)


"Inna Lillahi wa Inna Ilaihi Raaji'un"
Mungu Ailaze Roho ya Marehemu Hassan Kukuru kwa Amani - Amen