Monday, November 28, 2011

KATIKA KUSHEREHEKE MIAKA 50 YA UHURU - BIAFRA SPORTS CLUB YAKUSUDIA KUFANYA USAFI WA MAZINGIRA NA KUTOA MISAADA KATIKA HOSPITALI YA MWANANYAMALA TAREHE 9 DISEMBA, 2011

BAADHI YA VIONGOZI WA KLABU ZA BIAFRA, NAMANGA NA KUNDUCHI KWANZA

Klabu ya michezo ya Biafra kwa kushirikiana na klabu za michezo za Namanga na Kunduchi Kwanza wanawakaribisha wanamichezo, wadau wa michezo na wananchi kwa ujumla katika zoezi la kufanya usafi wa mazingira pamoja na kutoa misaada katika hospitali ya Mwananyamala ambayo ni Hospitali ya wilaya ya Kinondoni.

Zoezi hilo la kufanya usafi na kutoa misaada katika hospitali hiyo ni katika kutimiza wajibu wetu kama jamii hasa katika kusherehekea miaka 50 ya uhuru wa Tanzani ambao kilele chake kitakuwa tarehe 9 Disemba, 2011. Kamati teule ya maandalizi ya shughuli hiyo inakaribisha maoni, mapendekezo, ushauri, michango na misaada kutoka kwa watu wote watakaoguswa na dhamira hii kwa kuwasiliana na Katibu wa Biafra Sports Club ndugu Yahya Poli: +255 715 253 653, au tuandikie barua pepe biafra.jsclub@gmail.com

Kauli mbiu ya sherehe za miaka 50 ya uhuru kwa mwaka huu 2011 ni TUMETHUBUTU, TUMEWEZA, TUNASONGA MBELE! MICHEZO NI AFYA, MICHEZO USHIRIKIANO, MICHEZO NI UMOJA! 

Wednesday, November 09, 2011

HAFLA YA SHUKRANI ILIYOANDALIWA NA BIAFRA SPORTS CLUB YAFANA SANA

Siku ya Ijumaa tarehe 4/11/2011 kulikuwa na hafla ya kupongezana ambayo iliandalia kwa pamoja na ya Biafra Sports Club  na 90 Degrees Pub Kinondoni. Kupongezana huko kulitokana na kukamilisha mchakato wa kuandaa/kuandika katiba ya Biafra Sports Club ambapo zoezi hilo lilifanyika kwa ushirikiano na msaada mkubwa sana wa mawazo na maoni toka kwa klabu rafiki za Namanga Jogging Club pamoja na Kunduchi kwanza Jogging Club.  

Wadau wakibadilishana mawazo wakiongozwa na Ally Masharubu mwenye kaptula

wageni toka Namanga Jogging na Kunduchi Kwanza Joggin walianza kuwasili ukumbini saa 12 jioni huku wanabiafra wakiwakaribisha kwa bashasha na majadiliano ya hapa na pale katika kuboresha klabu zetu za jogging
 
wadau wa Namanga na Biafra Jogging wakibalishana mawazo kabla ya kuingia ukumbini

Richie Richie mzee wa Riddy Sound "in the house" alitoa burudani ya nguvu kwa wadau waliohudhuria hafla hiyo ambapo alicheza nyimbo mbalimbali na kukonga nyoyo za watu wote ukumbini ambapo kila mara watu walisimama kucheza na kushangili kwa nguvu.
Richie Richie akiwazungusha wadau
Wadau wakiwa na furaha tele huku wakiburudishwa na muziki wa Richie Richie

ukawadia wakati muafaka wa kutoa shukrani kwa klabu rafiki za Namanga Jogging na Kunduchi Kwanza Jogging pamoja na wadau wote waliowezesha kukamilika kwa katiba ya Biafra Sport Club ambapo kwa niaba ya viongozi na wanachama wa Biafra Sports Club Katibu wa Biafra Sports CLub alizungumza machache ya kuwashukuru na pia alikabidhi bahasha zenye andiko rasmi la shukrani kwa viongozi wa Namanga Jogging na Kunduchi kwanza Jogging Club kama inavyookana kwenye picha hapo chini.
Makatibu paleeeeee Mbusilo Joseph (Kunduchi Kwanza Jogging) Kaka Poli (Biafra Sport Club)

Viongozi wa Namanga Jogging na Kunduchi Kwanza Jogging baada ya kukabidhiwa Bahasha

Katika kumalizia hafla na itifaki kadhaa, burudani na shangwe ziliendelea mpaka majogoo kama anavyoonekana Makamu mwenyekiti wa Biafra Jogging - Mollel aka Mutu hapo chini.
Makamu Mwenyekiti wa Biafra Sports Club (mwenye suti) Abdul Mollel

Wednesday, November 02, 2011

KARIBU UPATE BURUDANI YA RIDDY SOUND SIKU YA IJUMAA TAREHE 4/11/2011 NDANI YA 90 DEGREES PUB KINONDONI

RICHIE RICHIE - MZEE WA RIDDY SOUND IN THE HOUSE

Baada ya mchakato wa kuandika Katiba ya Biafra Sports kukamilika, wanachama wa Biafra Sports Club kwa kushirikiana na uongozi wa 90 Degrees Pub (ambapo ndipo makao makuu ya klabu) unayofuraha kuwaalika wananchi wote na wana-jogging toka klabu za Temeke, Kunduchi, Namanga, Makongo na kwingineko tujumuike pamoja na kupata burudani ya muziki mwanana toka katika bendi ya Riddy Sound chini ya uongozi wa Richie Richie (pichani juu). Burudani hiyo itaanza saa 1 kamili usiku na kuendelea. Karibuni tupongezane baada ya kazi ngumu na muhimu!!!!!!
ENEO LA TUKIO - 90 DEGREES PUB

WOOOOOOOOOOOOOOTE MNAKARIBISHWA