Siku ya Jumapili, tarehe 4 Disemba, 2011 katika hafla ya uzinduzi wa Royal Billy's Lodge ambayo ipo nyuma ya Kanisa KKKT Tangi-Bovu palifanyika pia harambee kwa ajili ya kuchangia shughuli ya kufanya usafi wa mazingira katika Hospitali ya Mwananyamala pamoja na kutoa misaada ya hali na mali kwa wagonjwa katika wodi ya wazazi na wodi ya watoto hospitalini hapo. Kabla ya kuanza kwa hafla ya uzinduzi wa lodge hiyo na harambee, wakimbiaji wa mbio za pole pole (jogging) kutoka vilabu vya Biafra, Namanga, Kunduchi, Mbezi Beach, Temeke na wenyeji Tangi Bovu walikimbia mbio hizo kutoka Tangi Bovu kupitia Kawe na kurudi Tangi Bovu.
Baada ya mbio za pole pole kumalizika wakimbiaji waliendelea kufanya mazoezi kwa mtindo wa aerobics na kama kawaida ili aerobics inoge basi unapigwa muziki na kaka Michael J almaarufu Mopao anaongoza mazoezi hayo
Mmoja wa wakurugenzi wa Royal Billy's Lodge ndugu Tobias Owur akiingia wa mwisho baada mbio za pole pole - wakimbiaji wengi hawakumaliza mbio kwa kukimbi kama zilivyoanza.
Wana-jogging wengine walifikia vitini kama anavyoonekana kaka Mustafa Muro
Kutoka Kushoto ni Mama Kenisha Mkurugenzi wa Biafra Sports Club, Tobias Owur mmoja wa wakrugenzi wa Royal Billy's Lodge na Abdul A. Mollel Mwenyekiti wa Biafra Sports Club
wana-jogging wengine waliona viatu ni vizito na havivaliki tena
Dada Edita wa Namanga Jogging akinyoosha kiuno baada ya mbio
Wakiwakilisha Biafra - Kutoka kushoto Jacqueline Mugalura, Yahya Poli na Ally Masharubu
Mbusilo Joseph - katibu wa Kunduchi Kwanza pamoja na KP wa Temeke Jogging
Noah Machaka wa Biafra
Baada ya kumaliza mbio na burudani za hapa na pale, wana-jogging waliingia ukumbini kwa ajili ya kuanza harambee. Ndugu David Mwaka ambaye ni Mwenyekiti wa Namaga Jogging na Mkurugenzi wa Esoshi General Trading akiwakaribisha wageni ukumbini
Katibu wa kamati ya maandalizi akiweka mambo ya teknolojia sawa sawa akiwa sambamba a mhamasishaji wa kamati toka klabu ya namanga Charles Juma
Mdau Henry Byarugaba akiingia ukumbini, yeye pamoja na mchango wa fedha ameongeza pakiti 100 za maziwa ya Tanga Fresh toka kwenye idadi ya awali ambayo 400 hivyo kufikisha idadi ya pakiti 500
Mhamasishaji wa kamati Charles Juma alipigishwa magoti na kugombolewa ambapo pesa iliyopatikana iliongezewa kwenye mahitaji ya kukamilisha shughuli hiyo.
Bwana Benson Simba akiwasilisha ahadi ya Royal Billy's Lodge na Dabenco Enterprises ambao wamechangia fedha taslimu pamoja na fulana kwa ajili kuvaliwa siku hiyo.
Tobias Owur Almaarufu mkenya (mwenye miwani) akiwasilisha mchango wake
Mama Kenisha akipiga makofi baada ya kuahidi kuchangia fedha tasilimu pamoja na katoni kadhaa za sabuni
Mama Kenisha na Tobias Owur wakisoma ujumbe mfupi wa maandishi toka kwa wadau walio nje ya ukumbi ambao nao wameahidi kuchangia zoezi hilo
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi Abdul Mollel sehemu ya fedha zilizokusanywa papo hapo kwenye harambee
Baada ya harambee kumalizika na Charles kugombolewa ilikuwa ni vicheko na furaha tele kama wanavyoonekana mama Kenisha, Mopao na Charles mwenyewe wakicheka kwa furaha
Katibu wa kamati ya Maandalizi akiteta na wadau mbalimbali
Meza iliwakilishwa na Mollel ndugu Joseph Mwaka (katikati) na Mjomba Ole
Katika picha ya pamoja ni wana-jogging