Tarehe 7 Disemba, 2014 Tanzania ilishuhudia wanariadha toka mataifa mbalimbali duniani wakishiriki katika mashindano ya riadha yajulikanayo kama Uhuru Marathon ambayo ambayo kilele chake kilifanyika katika viwanja vya Leaders Kinondoni, Dar es Salaam. Fabian Joseph aliibuka kinara wa mashindano hayo ambayo mgeni rasmi alikuwa waziri wa michezo mheshimiwa Dr. Fenella Mukangara.
|
Waziri wa Michezo, Habari na Utamaduni Dr. Fenella Mukangara (picha kwa hisani ya Issa Michuzi) |
Zaidi ya kushiriki kama timu katika mashindano hayo, klabu ya michezo ya Biafra ilishiriki katika maandalizi ya mbio hizo kwa kushirikiana kwa karibu na wandaaji katika kupata washiriki toka katika vilabu vya jogging nchini Tanzania ambapo vilabu kadhaa vya jogging vilijitokeza.
|
Wanabiafra katika picha ya pamoja na wanajogging |
Klabu ya michezo ya Biafra ilitoa washiriki zaidi ya 10 katika mashindano hayo kwa ngazi mbalimbali kama vile 3, 5 na 21km. Ambapo baadhi yao Juma Ramadhani, Aziza Mwaimu, Zein Ahmed, Noha Machaka na Boniface Mangasala walishiriki katika mbio za 21km.
|
Wanabiafra waliokimbia 21km katika picha ya pamoja huku wakionesha vyeti vyao kutoka kushoto Zein Ahmed, Aziza Mwaimu, Noha Machaka na Juma Ramadhani |
|
Noha Machaka alishindana 21km akionesha cheti chake cha ushiriki. |
|
Zeinin Ahmed (aliyelala) akichuliwa msuli |
|
Wanabiafra katika picha ya pamoja baada ya mashindano wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wao Ms. Jaqueline Barozi (watatu toka kushoto) |
|
Asha Yusuph na Zein Ahmed wakionesha cheti cha ushiriki cha Zein |
|
Wanabiafra Emima George Madumba na Zein Ahmed |
|
Mwanabiafra Aziza Mwaimu akimaliza mbio |
Katika kilele hicho pamoja na washiriki toka katika klabu ya michezo ya Biafra kutoa ushindani kwa wanariadha wengine kulikuwa na changamoto mbalimbali zilizojitokeza kama vile kutopima afya kabla ya mashindano na kukosa uzoefu wa mashindano hayo.
Baada ya kujifunza changamoto hizo Kamati ya Utendaji ya Klabu ya Michezo ya Biafra imeweka mkakati mahususi wa kuwawezesha wanachama wake kushiriki kikamilifu katika mashindano yajayo.
Akiongea na blogu hii baada ya mashindano hayo, Mwenyekiti wa Klabu ya Michezo ya Biafra ndugu Abdul Mollel aliwashukuru waandaaji kwa kuwawezesha wanajogging kushiriki mbio hizo na vile vile kwa klabu yake kupata nafasi ya kuratibu ushiriki wa vilabu hivyo katika mashindano hayo.
|
Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Biafra Henry Maseko (kushoto) na Ayoub Layson |
|
Mwenyekiti wa klabu ya michezo ya Biafra (mwenye kofia) akiwapanga vijana wake |