Monday, December 24, 2012

SALAAM ZA KRISMASI NA MWAKA MPYA TOKA BIAFRA!

Wakati wakristo wakiwa katika maandalizi ya sikukuu ya kuzaliwa mwokozi, Yesu kristo mnamo tarehe 25 Disemba pamoja na maandalizi ya kuuaga mwaka 2012 na kuukaribisha mwaka 2013, klabu ya michezo ya Biafra inapenda kuwatakia wanachama, wapenzi, mashabiki pamoja na wadau wote wa michezo krismasi njema pamoja na heri ya mwaka mpya 2013.

Katika kipindi hiki cha mapumziko ya sikukuu, mazoezi yataendelea kila jumapili kama kawaida! Karibuni wote.

Wednesday, December 05, 2012

HABARI MCHANGANYIKO ZINAZOHUSU VILABU MBALIMBALI VYA JOGGING MKOA DAR ES SALAAM

Mwezi disemba ndio umeingia. Katika mfumo wa kupeana taarifa mbalimbali zinazohusu klabu zetu zinazojihusisha na mchezo wa mbio za pole pole (jogging), katika wiki ya kwanza na ya pili ya mwezi disemba kuna matukio kadhaa yaliloyofanyika na yatakayofanyika. Kama ilivyo ada, klabu ya michezo ya Biafra ilijumuika pamoja na klabu ya Namanga katika na kufanya mazoezi ya pamoja jumapili ya tarehe 2 Disemba. 

Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Ally Selemeani (mwenye bukta nyeusi) akiiwakilisha vyema Biafra
Mazoezi hayo yaliyofanyika kuzunguka barabara na mitaa mbali ya Namanga na Msasani yalianzia na kumalizikia Leecars Pub ambapo ni makao makuu ya klabu ya Namanga. Mara baada ya mazoezi ya pamoja, wanamichezo wote walijumuika na kujadiliana machache kwa ajili ya maendeleo ya klabu zote ikiwemo pea kupashana taarifa mbalimbali.

Kule Magomeni nako, klabu za Mzimuni na Taifa Jogging zilikutana na kufanya mazoezi ya pamoja ya mbio za pole pole na kisha kucheza mechi za mpira wa miguu (wanaume) na mpira wa pete (wanawake). Picha zote za michezo kati ya Taifa na mzimuni Jogging ni kwa hisani ya Taifa Jogging.
Wana Taifa na Mzimuni Jogging kwenye mchakamchaka

Kipindi cha mapumziko kwa mechi ya mpira wa miguu wanaume

Wachezaji wa mpira wa pete kutoka Taifa Jogger katika picha ya pamoja

Klabu ya michezo ya Namanga imejiandaa kufanya mkutano mkuu wa mwaka wa wanachama wake mnamo tarehe 9 Disemba, 2012. Akitoa taarifa ya kufanyika kwa mkutano huo mbele ya makatibu wa vilabu vya Biafra, Msasani na Kunduchi Kwanza, Katibu Mkuu wa Namanga ndugu Mangole alieleza kuwa mkutano huo unatarajiwa kufanyika katika ukumbi wa Ndege Beach nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam. Maandalizi ya mkutano huo yanaendelea. Alieleza kuwa vilabu rafiki vyote vitaalikwa kuhudhuria mkutano. 
Mwenyekiti wa namanga Sports Club ndugu David Mwaka (aliyesimama) akichangia mada kwenye kikao cha maandalizi ya mkutano mkuu: Picha kwa hisani ya John Badi)
 Kwa habari zaidi kuhusu mkutano huo bofya hapa.

TUNAWATAKIA WANA NAMANGA MKUTANO MKUU WENYE MAFANIKIO

Saturday, December 01, 2012

1.12. 2012: SIKU YA UKIMWI DUNIANI

Tangu Disemba 1, 1988 dunia imekuwa ikiadhimisha siku ya UKIMWI duniani. Wazo la kuadhimisha siku hiyo lilitolewa na James W. Bunn naThomas Netter ambao walikuwa ni maofisa habari (Global Programme on AIDS) kwenye Shirika la Afya Duniani. Dhumuni la kuadhimisha siku hiyo ni kutoa fursa kwa watu duniani kote kuungana katika mapambano dhidi ya VVU
Utepe Mwekundu
Huu ni wakati muafaka kwa jamii nzima wakiwemo wanamichezo pia kutafakari juu ya janga la UKIMWI. 

UKIMWI UNAUA! CHUKUA HATUA SASA, JILINDE NA MLINDE MWENZAKO PIA.