Tuesday, August 30, 2011

RATIBA YA HAFLA

BIAFRA JOGGING & SPORTS CLUB – 90 DEGREE PUB KINONDONI


RATIBA YA HAFLA YA KUJUMUIKA PAMOJA NA WATOTO KATIKA KUSHEREHEKEA SIKUKUU YA IDD MOSI, UKUMBI WA 90 DEGREES PUB KINONDONI - AGOSTI, 2011


MUDA
TUKIO
07:00 – 08:00
Wadau wote kuwasili klabuni na maandalizi ya kuanza kukimbia
08:00 – 09:00
Uzinduzi wa mbio
09:00 – 09:30
Chai kwa watoto
09:30 – 10:30
Kuwasili uwanjani na kuanza michezo mbalimbali
10:30 – 11:00
Kurudi klabuni na kuwasili kwa mgni rasmi
11:30 – 11:45
Kusomwa Risala ya watoto
11:45 – 12:30
Burudani ya nyimbo na maigizo toka kwa watoto
12:30 – 12:45
Risala na maelezo mafupi ya klabu
12:45 – 01:00
Maneno machache toka kwa mgeni rasmi (kujibu risala)
01:00 – 01:45
Mashindano mbalimbali ya watoto (chemsha bongo, kucheza, n.k.)
01:45 – 02:45
Chakula cha mchana na burudani
02:45 – 03:00
Burudani na maandalizi ya zawadi
03:00 – 03:30
Kugawa zawadi kwa watoto walioshiriki mashindano
03:30 – 04:00
Burudani ya muziki kwa watoto
04:00 – 04:30
Watoto kuondoka


KARIBU SANA, JUMUIKA PAMOJA NA WATOTO KWA UPENDO, FURAHA NA MATUMAINI

MWALIKO WA HAFLA YA KUJUMUIKA PAMOJA NA WATOTO WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU/HATARISHI ILI KUSHEREHEKEA SIKUKUU YA IDD MOSI, 2011

Ndugu,

Rejea muktadha uliobainishwa hapo juu;

Klabu ya Biafra Jogging kwa kushirikiana na 90 Degree Pub ya kinondoni katika kusherehekea sikukuu ya Idd wameandaa hafla ya kuwakaribisha watoto wanaoishi katika mazingira magumu/hatarishi kutoka vituo mbalimbali wilaya ya Kinondoni ili kujumuika nao katika michezo na chakula cha mchana. Lengo la shughuli hiyo ni kuwapa faraja na kuwaonyesha moyo wa upendo watoto hao katika siku hii muhimu na siku nyinginezo.
Hivyo basi, kwa heshima na taadhima tunachukua fursa hii adhimu kukualika rasmi katika hafla hiyo. Shughuli itaanza saa 1 asubuhi hadi jioni na itafanyika katika ukumbi wa 90 ̊ Pub Kinondoni iliyopo mtaa wa Isere Kinondoni ambapo pia ndipo makao makuu ya Biafra Jogging and Sports Club.
Ni matumani yetu kwamba utashiriki nasi na kutoa mchango wako ili kufanikisha shughuli yetu siku hiyo.
Tunakushukuru,
BIAFRA JOGGING AND SPORTS CLUB

………………………………………
MWENYEKITI