Tuesday, September 09, 2014

KLABU YA MICHEZO YA BIAFRA YASHIRIKI KATIKA UZINDUZI WA HUDUMA YA MIKOPO KWA WANACHAMA WA LAPF INAYOFAHAMIKA KAMA "PIGA KITABU NA LAPF"

Mfuko wa hifadhi ya jamii wa LAPF kwa kuzingatia umuhimu wa kuwawezesha wanachama wake kupata fursa ya kujiendeleza kielimu bila ya kuathiri kipato cha mwanachama, imezindua huduma mahususi ya mikopo ya elimu kwa wanachama wake inayojulikana kama "PIGA KITABU NA LAPF". Hafla ya uzinduzi wa huduma hiyo ilifanyika katika ukumbi wa LAPF Towers kijitonyama na uliwakusanya pamoja wadau mbalimbali wa LAPF ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Waziri wa Nchi, ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI, mheshimiwa Hawa Ghasia (Mb.)
 
Mgeni Rasmi akihutubia wadau wa LAPF (picha kwa hisani ya Michuzi Jr)
 
Mgeni rasmi pamoja na viongozi wa LAPF wakishuhudia fataki za uzinduzi
Mgeni Rasmi akimkabidhi mfano wa hundi mmoja wa wanachama wanufaika wa huduma ya piga kitabu na LAPF



Baadhi ya wanabiafra, kutoka kulia ni Yahya poli, Asha Yusuph, Salma Mathia, Ally S. Madulika
 
Wanabiafra wakipata mlo

Mweka Hazina wa Biafra ndugu Ayoub Layson (mwenye suruali ya kaki na shati jeusi) akisakata rhumba