Tuesday, June 18, 2013

WANABIAFRA WAADHIMISHA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA JUNI 16, 2013 KWA KUTEMBELEA KITUO CHA MAMA TEREZA MBURAHATI NA KUSHIRIKIANA NA WATENDAJI WA KUTO HICHO KUFANYA USAFI, KUCHEZA NA WATOTO NA KUTOA MISAADA YA KIBINADAMU KITUONI HAPO

Katika kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika tarehe 16 juni, 201 wanamichezo toka katika klabu ya Biafra waliamua kutembelea kituo cha kulelea wasiojiweza cha "Missioneries of Charity (Mother Teresa) Children's Home" Mburahati Madoto maarufu "Kwa Mama Tereza". Lengo la kutembelea la safari hiyo lilikuwa ni kujumuika pamoja na watoto wanaolelewa kituoni hapo na kutoa misaada ya kibinadamu kama vile chakula, mavazi na vifaa vya shuleni na pia kushirikiana na watendaji wa kituo hicho katika kazi mbalimbali kama vile kufanya usafi, kufua na kuwakutanisha watoto wanaolelewa kituoni hapo na watoto wenzao ili kuwa na wakati mzuri na kufurahi pamoja kucheza. 

 
Watoto wa Biafra wakiingia kwa Mama Tereza

Wanabiafra wakiingia kwa Mama Tereza
Safari ya kuelekea Kituoni hapo Ilianza saa 1:30 asubuhi kwa basi kupitia brabara ya Kawawa kisha Kigogo njia panda ya Tabata Dampo ambapo wanamichezo waliteremka hapo na kuanza mbip za pole pole kuelekea Mburahati Madoto kilipo kituo. Mara baada ya kuwasili na wanamichezo walipokelewa na Kiongozi wa kituo Sister Saviona ambaye tulimkabidhi misaada tuliyokuja nayo.   


Mratibu wa zoezi la ukusanyaji misaada Bi. Mariam Sabaje akiipanga mara baada ya kukabidhi
Zoezi la kutupa taarifa mbalimbali za kituo hicho lilifanyika na hatimaye tulipata fursa ya kuwasabahi watoto wanaolelewa kituoni hapo pamoja na watu wengine wakiwemo wazee na wafanyakazi.
Katibu Mkuu wa Biafra Yahya Poli akimsikiliza kwa makini Sister Saviona

Wanabiafra wakisikiliza historia ya Kituo cha Mama Tereza toka kwa Sister Saviona (hayupo pichani)

Katibu wa Kamati ya Ufundi Ally Juma akiongoza msafara kutembelea maeneo mbalimbali kituoni hapo

Baadhi ya watoto wanaolelewa kituoni wakichangamana na Wanabiafra

Hamza Kimathy akiwa na mtoto

Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Biafra - Ally Selemani pamoja na watoto

Ally Juma




Watoto wakifurahi picha

Mhamasishaji na mwimbishaji wa Biafra Chriss Matembo (wa pili kushoto waliosimama) akiwa na Makamu Mwenyekiti na watoto

Mara baada ya kutembezwa maeneo mbalimbali na kuwasalimia watoto kazi mbalimbali zilianza kufanyika ikiwemo kufua, kufagia na kupiga deki, kufuta vumbi madirisha na pia kupiga hadithi na watoto, fuatilia matukio yote kwenye picha. 
Kutoka kushoto; Mwajuma Mohamed, Zawadi Rajab, Emmy msechu na Mariam Sabaje

Abdallah Omari (kulia) na Ibrahim Kilasa

Chriss Matembo

Vijana wakifua


Magreth Warisanga (mwenye kofia) akifua pamoja na Jaqueline Barozi

Nancy Raphael (kushoto) akisaidiana kufua

Salma Mathias aifuta dirisha


Zawadi Rajab (mwenye kitambaa) na Mariam Sabaje wakipiga deki

Salma Mathias akisuuza nguo


Henry Maseko

Makamu M/Kiti Jqueline Barozi akianika nguo

Rehema Shaban na Miriam Joseph wakinika nguo

Watoto wakicheza pamoja

Mossi Said akiwahidithia hadithi kwa watoto
Zoezi la kufanya usafi lilikamilika na wakati wa mapumziko wanabiafra waliutumia vyema kujadiliana mambo mbalimbali waliyojifunza kituoni hapo pamoja na kuzungumza na wazee wanaoishi kituoni. 



Hatimaye siku maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika kwa mwaka 2013 kwa wanabiafra yalikamilika majira ya saa 6:30 mchana kwa kuwashukuru wahusika wote katika Kituo cha Mama Tereza kutukubalia ombi letu la kuwatembelea na pia uongozi pamoja na wafanyakazi na watoto kituoni hapo walitoa shukrani kwa kuwa pamoja nao na kuomba tuwe na utaratibu wa kwenda mara kwa mara. Baada ya shukrani, safari ya kurudi klabuni ikaanza  kwa mwendo mdogomdogo hadi njia panda ya Madoto na kisha kupanda gari. 



Kwa niaba ya Kamati ya Utendaji ya Klabu ya Michezo ya Biafra, napenda kuchukua fursa hii kuwashukuru wanachama wote kwa kujitolea vitu mbalimbali na kujitokeza kwa wingi. Vile shukrani za dhati ziwaendee wadau wetu Janice Mlunde na Faraja Emmanuel kwa kujitolea nguo kadhaa za watoto pamoja na sukari.
 

Tuesday, April 23, 2013

TIMU YA SOKA YA VIJANA YA BIAFRA (BYFT) KUCHEZA MECHI YA KIRAFIKI DHIDI YA ETTIHAD FC KATIKA UWANJA WA S/M M'NYAMALA B LEO

Katika kujiandaa na michuano ya Copa Coca Cola na BIafra Cup, timu ya soka ya vijana ya Biafra, leo inakutana na Ettihad FC katika mechi ya kujipima nguvu itakayochezwa katika uwanja wa shule ya msingi Mwananyamala B majira ya saa 10:00 jioni.
Baadhi ya wachezaji wa BYFT wakipasha misuli joto

Golikipa wa BYFT Godwin maarufu Subwoofer


BYFT katika picha ya pamoja na viongozi wao

Shime wadau, wapenzi na mashabiki wa soka hasa la vijana tujitokeze kwa wingi katika kushuhudia mechi hiyo.

Friday, April 19, 2013

NI MUHIMU KUUANDAA MWILI KWA AJILI YA MAZOEZI

Mlezi (Patron) wa klabu ya FAITA JOGGING ndugu Mustafa Mgawe ametukumbusha kwenye ukuta wake wa facebook. Soma hapa chini.

 

Thursday, April 18, 2013

BLOGU YA BIAFRA YATEMBELEWA ZAIDI YA MARA 600 KWA MWEZI MACHI NA APRILI, 2013

Klabu ya michezo ya Biafra  inatoa shukrani kwa watu wote kutoka mataifa mbalimbali duniani kwa kutembelea blogu yake. Katika kipindi cha mwezi mmoja tangu tarehe 20 Machi hadi leo 18 Aprili, 2013 imetembelewa zaidi ya mara 600 na watu kutoka Tanzania, Marekani, Urusi, Uingereza, Oman, Ujerumani, Ufaransa, Brazili, China na Sweden.
Takwimu za leo

Akizungumzia takwimu hizo, Katibu Mkuu wa klabu hiyo ndugu Yahya Poli alibainisha zaidi kwamba blogu hiyo imetembelewa zaidi ya mara 8000 tangu kuanzishwa kwake na pia alitoa wito kwa makampuni na wafanyabiashara kutumia blogu hiyo kutangaza bidhaa zao.

Sunday, April 14, 2013

BIAFRA YAANZA MCHAKATO WA KUANZISHA TIMU YA MPIRA WA PETE

Idara ya wanawake katika Klabu ya Michezo ya Biafra inawahamasisha na kuwaalika wasichana na wanawake wenye vipaji vya mchezo wa mpira wa pete (Netball) na mpira wa miguu kujiunga na klabu na kisha kuanzisha timu. Akizungumza na blogu hii mmoja wa waratibu wa zoezi hilo Bi. Aziza Mwaimu (pichani chini) alibainisha kuwa miongoni mwa wanachama wa klabu hiyo kuna ambao wanapenda kushiriki michezo ya aina mbalimbali hivyo fursa ya kuanzisha timu ni ya kipekee kwao kushiriki michezo
Aziza Mwaimu akionesha kipaji cha kupiga danadana
Makamu M/Kiti wa Biafra Jaqueline Barozi (kulia) akikokota mpira
Kama unapenda kujiunga na timu ya wanawake ya Biafra wasiliana na Katibu Mkuu kwa anuani inayoonekana kwenye kiunganishi upande wa kulia wa blogu hii.

JOGGING YA WANABIAFRA JUMAPILI TAREHE 14 APRILI, 2013 YANOGA

Wanabiafra wengi, wakubwa kwa wadogo leo wamejitokeza mapema asubuhi kwa ajili ya jogging ambayo iliwakusanya pamoja zaidi ya wanamichezo 70. Jogging lianzia klabuni na kuingia barabara ya Kawawa kuelekea Moroko, kisha barabara ya Mwai Kibaki hadi Viktoria kuelekea Mwanayamala hospitali, Mwananyamala A hadi studio, Barabara ya Kawawa tena na kuishia klabuni. Baada ya kufika klabuni wanajogging walifanya 'aerobis kwa zaidi ya dakika 50 kisha kuendelea na shughuli nyingine. Futailia picha chini.
Chris Katembo akiimbisha na kuongoza



Tunawapongeza wanabiafra na wadau wengine wote wlaiojitokeza kwa mazoezi ya leo, tunawakaribisha wengine wengimjiunge na klabu yetu. 

WE, WE, MAZOEZI NI AFYA, ACHA KUJIACHIA!!!

Friday, April 12, 2013

NI UJERUMANI DHIDI YA HISPANIA KATIKA NUSU FAINALI YA LIGI YA MABINGWA ULAYA

Hatimaye nusu fainali ya ligi ya mabingwa ulaya 2013 itazikutanisha timu bora kabisa toka nchini ujerumani na spain. Droo ya nusu fainali hiyo imefanyika leo huko Nyon nchini Uswisi ambapo imedhihirika kuwa vinara wa ligi ya Ujerumani Bayern Munich ambao wanaongoza Bundesliga kwa pointi 75 watamenyana na FC Barcelona wanaoongoza La Liga kwa pointi 78 wakati Borussia Dortmund inayoshika nafasi ya pili Bundesliga ikiwa na pointi 55 itakwaana na Real Madrid ambayo inashika nafasi ya pili pia kwenye La Liga ikiwa na pointi 65.

Mechi ya kwanza katika kinyan'ganyiro hicho itachezwa katika dimba la Allianz Arena nchini Ujerumani ambapo Bayern Munich itawakaribisha FC Barcelona tarehe 23 Aprili, 2013  na siku inayofuata yaani tarehe 24 Aprili, 2013 katika dimba la BVB Stadion Dortmund, Borussia Dortmund itawakaribisha Real Madrid.

Mzunguko wa pili utachezwa tarehe 30 Aprili, 2013 katika uwanja wa Santiago Bernabeu ambapo Real Madrid itaikaribisha  Borussia Dortmund na tarehe 1 May, 2013 katika uwanja wa Camp Nou Barcelona itachuana vikali na Bayern Munich.



Wadau mbalimbali wa soka nchini Tanzania wameanza kubashiri timu zitakazokutana katika fainali ambapo katika ukurasa wake wa Facebook, mwandishi na mchambuzi mahiri wa michezo nchini hususani mchezo wa soka ndugu Shaffih Dauda ambaye pia ni mtangazaji wa kipindi cha michezo cha redio ya Clouds ameandika hivi: - 
 

 Wachezaji wa Timu ya Vijana ya Biafra (BYFT) nao wamebashiri hivyo hivyo katika ukurasa wao wa Facebook ambapo wanatabiri kwamba itaongezeka mechi nyingine ya watani jadi toka nchini hispania (El Classico) kwa mwaka 2013. 
 
Haya, sisi yetu macho, tunasubiri kipute hicho hadi fainali itakayopigwa katika dimba la Wmbley nchini Uingereza.