picha mzunguko
Tuesday, June 19, 2012
Monday, June 18, 2012
BIAFRA KIDS YAIZAMISHA TEMEKE KIDS KWA MABAO 3 - 0
Katika kujiweka fiti kwa ajili ya kushiriki michuano ya Winome mwezi Julai mwaka 2012, timu ya Biafra Kids ilichuana na Temeke Kids katika uwanja wa Zakheem Mbagala. Mechi hiyo iliyochezwa majira ya saa sita mchana ilishuhudiwa na watazamaji zaidi ya mia tano ambao ni wanamichezo kutoka katika vilabu mbalimbali vya michezo mkoani Dar es Salaam.
Kikosi kazi cha Biafra Kids
Mchezaji wa Soka Aziza (Biafra Ladies) mwenye suruali nyeusi akifuatilia mechi kwa makini
Biafra Kids wakitoka uwanjani kwa mapumziko
Pamoja na uwanja kuwa na michanga mingi, vijana walionyesha kandanda safi kiasi cha kushangiliwa muda wote na hadi mpira unakwisha Biafra Kids walikuwa washindi wa mechi hiyo kwa mabao 3 - 0.
VILABU KADHA VYA 'JOGGING' MKOA WA DAR ES SALAAM VYAKUTANA NA KUFANYA MAZOEZI YA PAMOJA NA TEMEKE JOGGING
Jumapili ya tarehe 17 Juni, 2012 ilikuwa ni siku njema kwa wanamichezo katika mkoa wa Dar es Salaam. Vilabu zaidi ya 15 vya michezo, hasa vinavyohamasisha mchezo wa mbio za pole pole "jogging" vilifanya mazoezi ya pamoja kwa mwaliko wa klabu kongwe ya Temeke. Wanamichezo zaidi ya mia sita walikusanyika katika uwanja wa Taifa na saa 12:30 asubuhi walianza safari ya kuelekea Mbagala katika ukumbi wa Dar-Live kisha katika viwanja vya Zakheem kwa mchezo wa mpira wa miguu.
Biafra Jogger wakiongoza msafara wa wana-jogger
Biafra Kids wakiongoza Biafra Jogger
Baadhi ya wanakunduchi Kwanza
Makamu Mwenyekiti wa Biafra Ms. Jacqueline Barozi akiingia Darlive
Mwenyekiti wa Biafra (mwenye bukta ya bluu) akishiriki aerobics
Wanabiafra walioshiriki mazoezi katika picha ya pamoja ndani ya Darlive Mbagala
Monday, June 11, 2012
BIAFRA JOGGING NDANI YA JEZI MPYA YAFANYA MAZOEZI YA PAMOJA NA NAMANGA NA KUNDUCHI KWANZA
Klabu ya michezo ya Biafra imezindua awamu ya kwanza ya uzinduzi wa jezi za mazoezi ya mbio za pole pole (jogging) kwa kufanya mazoezi ya pamoja na klabu za Namanga Jogging na Kunduchi Kwanza Jogging.
Wadada wa Biafra Jogging waking'aa ndani ya 'uzi' mpya
Jezi mpya ya Biafra Jogging inavyoonekana kwa nyuma
Wanamichezo wakikatiza maeneo ya polisi Oysterbay
Mazoezi hayo yaliyofanyika jana jumapili tarehe 10 Juni, 2011 yalianzia na kuishia katika klabu ya Namanga na wanamichezo walikimbia zaidi ya kilomita 8 kwa kupitia barabara za old Bagamoyo na Ali Hassan Mwinyi (Namanga, Oysterbay Polisi, Drive -Inn, Moroko, Viktoria, Sayansi, Rose Garden, Kwa Nyerere, Chama, Drive-Inn, Oysterbay Polisi na Namanga).
Wadada wa Kunduchi Kwanza waking'aa pia na uzi wao
Viongozi wa klabu zote 3 walikutana
MATUKIO KATIKA MECHI YA BIFRA KIDS DHIDI YA KOMBAINI YA KINONDONI
Katika kujiimarisha zaidi na kuongeza uzoefu wa mechi ngumu, timu ya Biafra Kids ilipokea na kukubali mwaliko wa kucheza na timu ya kombaini ya mkoa wa Kinondoni ambao wameteuliwa kutoka katika timu mbalimbali zilizoshiriki michuano ya Copa Coca Cola kwa vijana walio chini ya umri wa miaka 17 kanda ya Kinondoni. Mechi hiyo iliyochezwa katika viwanja vya Tanganyiksa Packers Kawe, siku ya J'mosi tare 9 Juni, 2012 illisha kwa Biafra Kids kupoteza mchezo huo baada ya kufungwa mabao 2 - 1.
KIKOSI CHA BIAFRA KIDS
KOMBAINI YA KINONDONI
Kocha wa Biafra Kids William Masika (kushoto) akiwa na viongozi wa Kombaini
Tuesday, June 05, 2012
BIAFRA KIDS PLAYER OF THE WEEK 4 - 10 JUNE, 2012
From this week on, we'll be presenting you the club's player of the week. The said players is chosen by the players themselves, trainers and team captains. in order for the player to be selected a player of the week, he must demonstrate highest state of discipline on and off the field, follow and keep the instructions given by the trainers, demonstrate the ability and agility of playing footbal, e.t.c.
Players and leaders of Biafra Kids
And, the player for this week (4th - 10th June, 2012) is Ahmed Suleiman (pictured below). He joined the club in 2011. Ahmed is 16 years old studying at Hanasif Secondary School Form II. He is mong the players club enrolled in Copa Coca Cola under 17 tournament for Kinondoni Zone. His teammates calls him Mafisango because his kind of play resembles the late player who played for Simba 2011/12 season.
KLABU YA BIAFRA YAITISHA MKUTANO MKUBWA WA WANACHAMA, MASHABIKI NA WADAU WAKE
Katika harakati za kuiimarisha klabu, Mwenyekiti wa klabu ya Michezo ya Biafra Bw. Abdul Mollel, kupitia Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo ameitisha mkutano mkubwa ambao utawakutanisha wanachama wote, mashabiki na wadau wa klabu hiyo pamoja na wanamichezo kwa ujumla mnamo tarehe 8 Juni, 2012 siku ya ijumaa. Mkuktano huo unatarajiwa kuanza saa 12:30 jioni na kumalizika saa 2:30 usiku na utafanyika makao makuu ya klabu 90 Degrees Pub Kinondoni.
Mwenyekiti wa Biafra Abdul Mollel (kushoto) akiwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya klabu Ally Selemani almaarufu Masharubu
Wanabiafra wakiwa klabuni
Wanabiafra: kutoka kushoto; Robert Mwakibugi, Dastan Barozi, na mgeni wao klabuni
Akitoa taarifa za mkutano huo, Katibu Mkuu wa klabu ya Biafra alieleza kuwa pamoja na masuala mengine, ajenda za mkutano huo ni: -
- Kupata taarifa na kujadili maendeleo ya klabu
- Ushiriki wa wanabiafra katika shughuli mbalimbali za klabu vikiwemo vikao na mazoezi,
- Kupokea mpango kazi wa mwaka wa klabu (Juni - Disemba, 2012)
- Kugawa sare (uniform) kwa wanachama waliolipia.
Akitoa msisitizo, Katibu Msaidizi wa klabu Betwely Kyando (pichani chini) alieleza kuwa kikao hicho ni muhimu sana hivyo kila mwanachama, mshabiki na mdau wa Biafra anapaswa kuhudhuria bila kukosa kwa kuwa masuala yatakayojadiliwa yatasaidia harakati za kuimarisha klabu na mchakato wa kuleta maendeleo kwa wanachama kwa ujumla.
Betwely Kyando - Katibu Msaidizi, Biafra Sports Club
Kwa maelezo, maoni, ushauri, au ungependa kushiriki kwenye mkutano huo, wasiliana na Katibu Mkuu kwa barua pepe (biafra.jsclub@gmail.com) au kwa simu +255 715 253 653.
NYOTE MNAKARIBISHWA
Monday, May 21, 2012
MATUKIO BAADA YA MAZOEZI YA MBIO ZA POLE POLE KATIKA PICHA
Siku ya jumapili tarehe 20 Mei, 2012 klabu ya michezo ya Biafra ilizialika klabu za Taifa Jogging na Kawe Jogging pamoja na wadau wengine katika kufanya mazoezi ya pamoja ya mbio za pole pole 'jogging' ambazo zilianzia katika makao makuu ya klabu ya Biafra kupitia barabara ya Kawawa, Dunga, Peace, Mwin'juma, Kawawa tena na kumalizikia makao makuu ya Biafra.
Wanamichezo wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Taifa Jogging akitoa nasaha zake
Mazoezi hayo yalihudhuriwa na wanamichezo zaidi ya mia moja hamsini kutoka Temeke pamoja na Kinondoni ambapo yaliongeza hamasa hadi kupelekea watu wengine wajumuike pamoja huku nyimbo mbalimbali za kuhamasisha wakimbiaji zikiimbwa kwa ustadi mkubwa.
wanamichezo wakiimba na kucheza klabuni
Baadhi ya viongozi wa Biafra na Taifa jogging
Mashabiki wa soka nao hawakuwa nyuma kuonyesha ushabiki wao kwa kushangilia ushindi wa klabu ya Chelsea ambayo imenyakua ubingwa wa kombe la klabu bingwa ulaya kwa kuitandika sawasawa timu ya byern Munich ya ujerumani kwa mikwaju ya penati.
Wanabiafra Michael Silili (wa kwanza kulia) na Editha Tungara (wa mwisho) katika picha ya pamoja na Bi. Arafa nwenzake wakiiwakilisha Taifa Jogging
Hata mashabiki wa Liverpool nao walikuwepo
Mwanabiafra Editha Tungaraza
Ismail Hamad (kushoto) na Michaele Silili (kulia)
Akizungumza baada ya kumaliza mazoezi mwenyekiti wa Taifa Jogging alieleza kuwa wamefurahishwa sana na mwaliko wa kuja kufanya mazoezi ya pamoja kwa kuwa kutembeleana huku kutaimarisha sana uhusiano baina ya klabu rafiki, hivyo alitumia pia fursa hiyo kuwaalika Wanabiafra Temeke na kufanya mazoezi ya pamoja Taifa jogging pamoja na klabu nyingine.
Friday, May 18, 2012
BIAFRA SPORTS CLUB YAZIKARIBISHA KLABU ZA JOGGING ZA KAWE NA TAIFA KUFANYA JOGGING PAMOJA
Katika kuendeleza uhusiano na ujirani mwema mwema, klabu ya michezo ya Biafra inaendeleza programu yake endelevu ya kufanya mazoezi ya pamoja na klabu mbalimbali za jogging mkoani Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla. Programu hiyo iliyoanza kabla ya klabu kusajiliwa itaendelea tena jumapili ya tarehe 20 Mei, 2012 ambapo klabu ya Taifa Jogging ya Temeke na Kawe Jogging ya Kawe mzimuni watakuwa wageni wa klabu ya Biafra.
Baadhi ya Wana-Kawe jogging
Akithibitisha wa klabu ya Kawe ndugu Lazaro alieleza kuwa ni fursa nzuri kwa wanamichezo kukutana kwa apmoja mara kwa mara na kubadilishana mawazo pamoja na uzoefu wa namna ya kuziendeleza klabu zetu.
Klabu ya Biafra inawakaribisha wakaazi wote wa Kinondoni hasa wapenda mazoezi katika kufanya mazoezi ya pamoja siku hiyo n siku nyingine.
Thursday, May 17, 2012
MCHEZAJI NGULI WA ZAMANI YA TIMU YA TAIFA NA YANGA KUTEMBELEA MAZOEZI YA BIAFRA KIDS
Katika harakati za kuwapa fursa za kujifunza toka kwa wachezaji wa mpira wa miguu wa zamani, klabu ya Biafra imeanzisha programu maalumu ya kuwakutanisha wachezaji wa zamani na vijana hao. Programu hiyo inayoitwa 'inspired by the legends' itaanza rasmi juma hili na itafanyika takriban mara mbili kila mwezi.
mchezaji nguli (legend) mwenye bahati ya kufungua programu hiyo ni Edibiliy Jonas Lunyamila (pichani chini) ambapo atatembelea mazoezi ya Biafra Kids siku ya ijumaa tarehe 18, Mei, 2012 katika viwanja vya Biafra Kinondoni.
Edibily Jonas Lunyamila aka Lunya
Akizungumza juu ya ujio huo, kocha wa Biafra Kids William John Masika alieleza kuwa amefanya mawasiliano na mchezajihuyo na amethibitisha kuhudhuria mazoezi na baadaye kuzungumza na vijana hao. Pia atatumia fursa hiyo kutoa ushauri kwa viongozi wa namna ya kuwaendeleza vijana hao kwa kufuata misingi na miiko ya mchezo wa mpira wa miguu.
Kwa niaba ya viongozi, wanachama, wapenzi na mashabiki wa Biafra Sports Club, tnapenda kuchukua fursa hii kumkaribisha Lunyamila klabuni kwetu. Karibu sana!!!!
Sunday, May 13, 2012
THE JUNIORZ YASHINDA 2 -1 DHIDI YA VIJANA MUSLIM
Katika kusherehekea siku ya kina mama duniani (mother's day) leo, timu ya Biafra Kids almaarufu The Juniors wameichapa timu ngumu ya Vijana Muslim almaarufu 'dume' kwa mabao 2 -1 bila huruma katika michuano ya Copa Coca Cola kwa vijana walio chini ya umri wa miaka 17 kanda ya Kinondoni.
The Jrz wakipasha misuli moto kabla ya kuingia uwanjani.
Vijana Muslim nao wakipasha moto misuli kabla ya kuingia uwanjani
Dume ni moja kati ya timu zinazohofiwa sana kwenye michuano hiyo kwa kuwa ni timu yenye uzoefu wa kushiriki mashindano mbalimbali kwa muda mrefu huku The Juniorz wakiwa wageni kabisa kwenye mashindano hayo hali iliyopelekea mashabiki wengi kuipa nafasi kubwa timu ya Dume lakini katika hali ya kushangaza, The Juniorz waliwafundisha mpira Dume.
Kikosi kilichoanza - The Juniorz
Kikosi kilichoanza - Vijana Muslim
Baada ya kutandaza kandanda safi tangu sekunde ya kwanza ya mchezo, Biafra Kids walijiandikia bao la kwanza dakika ya 28 kupitia kwa winga wake machachari Babulu Nussura. Hadi mapumziko Biafra Kids walikuwa wakiongoza kwa bao 1.
Kiongozi wa Dume akiwa na majonzi ya kufungwa timu yake
Mchezo huo ambao pia ulishuhudiwa na wanasoka mbalimbali wa zamani (pichani chini) uliendelea tena kipindi cha pili ambapo timu ya Dume walijipatia bao la kusawazisha lilioleta utata ambapo wengi miongoni mwa watazamaji walilisisitiza kuwa mchezaji aliyefunga goli la Dume alikuwa ameotea na alionekana wazi kabisa kuwa ameotea. hata hivyo, The Juniorz hawakukata tamaa kabisa kwani pamoja na kuchezewa rafu nyingi hatimae waliandika bao la pili kwa njia ya penalti dakika ya 87 baada ya golikipa wa timu ya Dume kumchezea rafu mbaya kiungo machachari wa The Juniorz Hussein Tahiddin kwenye eneo la hatari. Penati hiyo iliwekwa kimiani na Rashid Sajji.
Golikipa wa zamani
Hadi mwisho wa mchezo Biafra Kids iliibuka kidedea na ushindi wa mabao 2 -1 wakiwa na pointi saba na magoli 8. Timu hiyo inarudi tena uwanjani jumatano tarehe 16 Mei, 2012 ambapo itacheza na timu ya Hanasif mchezo ambao utapigwa katika dimba la shule ya sekondari ya Muslim ambao ni uwanja wa nyumbani wa Dume.
Subscribe to:
Posts (Atom)
