Sunday, September 18, 2011

MATUKIO MBALIMBALI YA BONANZA LA KUNDUCHI KWANZA JOGGING KATIKA VIWANJA VYA KUNDUCHI MTONGANI 11/09/2011

Katibu wa Biafra Sports CLub Poli Yahya (mwenye fulana nyeupe) akiwa na mdau Issa Majaliwa



Mkurugenzi wa Biafra Sports Dada Nash (mwenye fulana nyekundu) akiwa na wanabiafra wakipanga mikakati ya mechi ya wanawake

Kikosi kamili cha mchanyato sports club

ni kama anasema "hapa mguuni, kuna goli 5"

ni kama wanasema "huyu anafunga wapi??? mbona goli liko huku!!"

Tumeshindaaaaaaaa!!

Taifa Queens ya Kunduchi, Namanga na Biafra Jogging!

NAMANGA JOGGING, BIAFRA JOGGING NA KUNDUCHI KWANZA JOGGING TAREHE 11/09/2011

Wadau wakipasha viungo kabla ya kuanza kwa mbio za pole pole

Michael a.k.a Mopao akiongoza 'warm up' kwa wakimbiaji katika viwanja vya kunduchi mtongani

BONANZA LA MBIO ZA TARATIBU KUNDUCHI MTONGANI TAREHE 11/09/2011

 Hussein Taiddin - Midfielder wa Biafra Kids Football Club

Wadau katika mbio za pole pole kuelekea Kunduchi Mbuyuni

Safari ya kuelekea Kunduchi Mbuyuni inaendelea

Monday, September 12, 2011

Rambi rambi za ajali ya meli znz

Wanachama wa klabu ya Michezo ya Biafra kwa kushirikiana na uongozi wa 90 Degrees Pub unatoa rambirambi zao kwa ndugu, jamaa, marafiki na kwa watanzania wote kwa ujumla kwa msiba uliolikumba taifa kutokana na ajali ya kuzama kwa meli ya Mv Spice huko Zanzibar na kuuwa watu zaidi ya 200.

Mwenyezi Mungu awape nguvu wafiwa wote na azilaze roho za marehemu wote mahala pema peponi Amen

Sunday, September 04, 2011

wadau wakilisakata rhumba la riddy sound



Mwenyekiti wa namanga sports club (mwenye shati la pink) akiwaongoza wadau kusakata rhumba

                                                             Kama kawaida yako - John, mbavu zangu mie!

                                                           watu wakijiandaa kuingia kwenye kikao
baada ya mbio ni .....

                                                 Mwenyekiti wa Kunduchi Kwanza Jogging Club akiwa na mweka Hazina wa Namanga Jogging Club

 Robert Mwakibugi katika maandalizi ya kikao


Geofrey

Dogo Janja hapa anasubiri (Michael Clement)

Saturday, September 03, 2011

wakati wa kuongeza pumzi

seki beleko akiongoza mbio na kuimbisha wadau

matukio mbalimbali ya tamasha la michezo katika picha

Bethwel Kyando (mwenye kofpia nyeupe) ambaye ni katibu Msaidizi akiimbisha wadau

Matukio mbalimbali ya hafla katika picha

baadhi ya watoto kutoka katika vituo mbalimbali wakifuatilia matuko kwenye tv


baadhi ya watoto kutoka katika kituo cha Hananasif

wadau wakijadili  jambo

Mzee Faustin Makima (mwenye kofia) almaarufu mzee Fambo akiongoza mbio

hata Twitter tupo

Kwa hesima na taadhima, klabu inawaarifu wadau wote kuwa twaweza kupashana habari kupitia mtandao wa twitter na anuani ya klabu ni twitter.com/biafrajogging

Karibuni.

Risala kwa waalikwa


Hapa tunatafuta kina Juma Ikangaa na Filbert Bayi

watoto wakijiandaa kukimbia

Jua lilee literemke mama!!!

Seki Beleko akiimbisha wana-jogging

Mchaka mchaka ...............

Tuesday, August 30, 2011

RATIBA YA HAFLA

BIAFRA JOGGING & SPORTS CLUB – 90 DEGREE PUB KINONDONI


RATIBA YA HAFLA YA KUJUMUIKA PAMOJA NA WATOTO KATIKA KUSHEREHEKEA SIKUKUU YA IDD MOSI, UKUMBI WA 90 DEGREES PUB KINONDONI - AGOSTI, 2011


MUDA
TUKIO
07:00 – 08:00
Wadau wote kuwasili klabuni na maandalizi ya kuanza kukimbia
08:00 – 09:00
Uzinduzi wa mbio
09:00 – 09:30
Chai kwa watoto
09:30 – 10:30
Kuwasili uwanjani na kuanza michezo mbalimbali
10:30 – 11:00
Kurudi klabuni na kuwasili kwa mgni rasmi
11:30 – 11:45
Kusomwa Risala ya watoto
11:45 – 12:30
Burudani ya nyimbo na maigizo toka kwa watoto
12:30 – 12:45
Risala na maelezo mafupi ya klabu
12:45 – 01:00
Maneno machache toka kwa mgeni rasmi (kujibu risala)
01:00 – 01:45
Mashindano mbalimbali ya watoto (chemsha bongo, kucheza, n.k.)
01:45 – 02:45
Chakula cha mchana na burudani
02:45 – 03:00
Burudani na maandalizi ya zawadi
03:00 – 03:30
Kugawa zawadi kwa watoto walioshiriki mashindano
03:30 – 04:00
Burudani ya muziki kwa watoto
04:00 – 04:30
Watoto kuondoka


KARIBU SANA, JUMUIKA PAMOJA NA WATOTO KWA UPENDO, FURAHA NA MATUMAINI

MWALIKO WA HAFLA YA KUJUMUIKA PAMOJA NA WATOTO WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU/HATARISHI ILI KUSHEREHEKEA SIKUKUU YA IDD MOSI, 2011

Ndugu,

Rejea muktadha uliobainishwa hapo juu;

Klabu ya Biafra Jogging kwa kushirikiana na 90 Degree Pub ya kinondoni katika kusherehekea sikukuu ya Idd wameandaa hafla ya kuwakaribisha watoto wanaoishi katika mazingira magumu/hatarishi kutoka vituo mbalimbali wilaya ya Kinondoni ili kujumuika nao katika michezo na chakula cha mchana. Lengo la shughuli hiyo ni kuwapa faraja na kuwaonyesha moyo wa upendo watoto hao katika siku hii muhimu na siku nyinginezo.
Hivyo basi, kwa heshima na taadhima tunachukua fursa hii adhimu kukualika rasmi katika hafla hiyo. Shughuli itaanza saa 1 asubuhi hadi jioni na itafanyika katika ukumbi wa 90 ̊ Pub Kinondoni iliyopo mtaa wa Isere Kinondoni ambapo pia ndipo makao makuu ya Biafra Jogging and Sports Club.
Ni matumani yetu kwamba utashiriki nasi na kutoa mchango wako ili kufanikisha shughuli yetu siku hiyo.
Tunakushukuru,
BIAFRA JOGGING AND SPORTS CLUB

………………………………………
MWENYEKITI