Wednesday, July 10, 2013

TANZIA TANZIA TANZIA

Juma lililopita limekuwa ni la huzuni kwa wanabiafra na tasnia ya mchezo wa mbio za pole pole (jogging) mkoa wa Dar es Salaam kwa ujumla. mwanzo mwa juma tulipokea taarifa ya msiba wa mke wa katibu Mkuu wa Temeke Jogging (Rasmi) ndugu Togocho ambapo mazishi yalifanyika maeneo ya kurasini Mivinjeni. Vilabu kadhaa vya jogging viliendelea kuonesha umoja kwa kushiriki kwenye msiba huo na mingine.
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Biafra Henry Maseko (mwenye shati jeupe) akitoa nasaha kwenye msiba wa mke wa ndugu Togocho


Siku ya Jumatano wanachama wa Biafra kundi la watoto Mtoro Elvis na kaka yake Jimmy Elvis (pichani chini)  nao walifiwa ni bibi yao mlezi ambapo mazishi yalifanyika huko Mlandizi mkoa wa Pwani.
Jimmy Elvis

Mtoro akiwa na kocha Willy
Huzuni iliendelea kutamalaki siku ya jumapili tarehe 7 Julai, 2013 ambapo alfajiri ya siku hiyo klabu ya michezo ya Biafra ilimpoteza mwanachama wake mtoto Aboubakar Iddi Maganga ambaye alifariki kwa ajali ya gari iliyotokea Kibaha mkoani Pwani. Taarifa ziliwafikia Wanabiafra wakati wakiwa katika mazoezi asubuhi hiyo toka kwa baba mzazi wa Aboubakar bwana iddi Maganga ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya Utendaji ya Biafra. Mazishi ya marehemu Aboubakar yalifanyika katika makaburi ya Kinondoni siku ya Jumatatu tarehe 8 Julai, 2013. 

Kaburi alimozikwa Aboubakar iddi Maganga
Baadhi ya waombolezaji




Kaka nathan akiiwakilisha Temeke Jogging



Wafiwa; Iddi maganga na mkewe


Waombolezaji


Rose Mwakibugi (mwenye rasta) pamoja na Asia Mohamed (mwenyekiti wa kunduchi kwanza)

Mwenyekiti wa Kopa Original Jogging  Mustapha alikuwepo
Tunamwomba Mwenyezi mungu azilaze roho za marehemu wote mahala pema peponi.

Sunday, July 07, 2013

KATIKA KUADHIMISHA SIKUKUU YA SABASABA, WANABIAFRA WAKIMBIA ZAIDI YA KILOMITA 8 JUMAPILI TEREHE 7 JULAI, 2013

Kama ilivyo ada ya kila jumapili kufanya mazoezi ya mbio za pole pole (jogging) pamoja, leo Wanabiafra wamekimbia zaidi ya kilomita nane katika kuadhimisha sikukuu ya saba saba. Mbio hizo zilianza majira ya saa 12:25 asubuhi yalipo makao makuu ya klabu kupitia barabara ya Kawawa hadi Moroko, barabara ya Kibaki hadi kwa Mwalimu Nyerere, barabara ya Rose Garden Hadi Sayansi, brabara ya Maji Machafu na kufuata barabara ya Akachube mpaka Peace Mwananyamala, barabara ya kwa Kopa, barabara ya Dunga hadi Hombus kisha barabara ya Kawawa hadi Msikiti wa Mtambani tukaingia "service road" ya upande Kinondoni Hospital mpaka Manyanya (Chimbinga) ambapo mbio ziliishia. Fuatilia matukio kwa picha mbalimbali!
Maeneo ya kwa Nyerere


Barabara ya kuelekea Rose Garden














Mwana- mzimuni Jogging (mwenye fulana ya kijani) aliungana na Wanabiafra kwenye mazoezi




Tukivuka mataa ya Sayansi kuelekea maji machafu

  
Tunawashukuru sana askari wa usalama barabarani (traffic) kwa kutambua mazoezi yetu, mara zote wamekuwa wakituwezesha kutumia na kuvuka barabara hasa sehemu zenye mataa kwa kusimamisha magari mpaka tunapopita. Leo wakati tukivuka njia panda ya sayansi, askari wa usalama barabarani alisimamisha gari zote tukiwa umbali wa takriban mita moja na nusu kabla ya kufika kwenye mataa. Tulivuka salama na kuendelea na mazoezi.

Watoto wakifurahia mazoezi kwa tabasamu

Tukinyoosha miguu na kupanga vyema mistari maeneo ya Akachube


Tukikatiza kuingia barabara/maeneo ya Peace - Mwananyamala



Tukinyoosha viungo baada ya kufika Chimbinga



Mwanachama mpya Bw. Khamis Seif (mwenye jezi nyekundu - aliyesimama) akitambulishwa





Watoto wakipata staftahi ya chai baada ya mazoezi
 
Rehema Shabani (kushoto) na Miriam Jospeh (kulia) baada ya mazoezi wakipata habari

Wanachama wapya Boniface (kushoto) na Hassan (kulia)



Wanabiafra wakiangalia picha za matukio ya jogging leo
Kwa niaba ya Kamati ya Utendaji, tunawapongeza Wanabiafra wote walioshiriki mazoezi siku ya leo na kusisitiza pia kuwahimiza wanachama wengine, ndugu, jamaa na marafiki zetu washiriki mazoezi ili kujenga afya zao.