Monday, March 11, 2013

KUNDUCHI KWANZA YAFANIKISHA MAZOEZI PAMOJA NA HARAMBEE TAREHE 10 MACHI, 2013

Jana tarehe 10 Machi, 2013 wanamichezo kutoka Kawe Beach, Kawe Social & Sports Club, Msasani Jogging & Sports Club, Naamanga Sports Club, Biafra Sports Club pamoja na wenyeji Kunduchi Kwanza walikusanyika pamoja na kufanya mazoezi ya mbio za pole pole (jogging) ambazo ziliwakutanisha zaidi ya wanamichezo 100 pamoja na wadau wengine. Mbio hizo zilianzia Makao Makuu ya klabu ya Kunduchi Kwanza Malanja kupitia mbuyuni, Afrikana, kipita shoto (round about) cha Kawe na kisha kurudia njia hiyo hiyo hadi Malanja. 
Kundi la Msasani  

Kundi la mwisho

Michael Juma aka Mopao (mwenye bukta nyeusi mbele) akiongoza Earobics 


Mara baada ya mazoezi ya mbio pamoja na aerobics, wanamichezo waliendelea kupata mapumziko mafupi na burudani mbalimbali zilizoandaliwa.
Mwenyekiti wa Biafra Abdul Mollel (mwenye bukta ya bluu) akijadiliana jambo na wadau

Wadau wakipata supu

Wenyeji Kunduchi Kwanza wakifuatilia matukio
Mwenyekiti wa Kawe Social and Sports Club almaarufu Mzee Risasi (menye fulana nyeupe akiwa na wadau
Baada ya mapumziko na burudani mbalimbali, wanamichezo walijumuika tena pamoja kwa ajili ya tukio mahususi kwa ajili ya siku hiyo ambapo wana Kunduchi Kwanza pamoja na wanamichezo na wadau wengine wote waliohudhuria walipata fursa ya kumpa pole Mmiliki wa Malanja Executive Inn ambaye pia ni mlezi na mdhamini wa klabu ya Kunduchi Kwanza baada ya kuunguliwa na ukumbi wa Malanja sehemu ambayo pamoja na kutumika kwa ajili ya matukio mbalimbali ya kijamii wana Kunduchi kwanza walikuwa wakiutumia kwa ajili ya mikutano yao. 
Wana Kunduchi Kwanza wakiwa kwenye mkutano ndani ya Malanja Hall kabla ya kuungua
Zoezi la kutoa pole lilifanyika pamoja na harambee ya kuchangia ujenzi wa ukumbi huo ambapo wanamichezo wote waliokuwepo walichangia kwa kadri ya uwezo na vilabu vyote vilivyoshiriki navyo vilichangia.  
MC akiwakaribisha Kunduchi Kwanza (pichani) kusalimiana na wadau

Wana Kunduchi Kwanza

Wana Kawe Social & Sports Club wakisalimia wadau 

wana Msasani Jogging wakiongozwa na Katibu Mkuu wao ndugu Mangula

Wana Namanga Sports Club 

Mwenyekiti wa Biafra Abdul Mollel akitoa pole za klabu yake

Sehemu ya pesa taslimu zilizochangwa mara tu baada ya kuanza harambee

Mweka Hazina wa Kunduchi Kwanza (kulia) akiwa na Malanja 

Kamati ya kusimamia zoezi la harambee wakijiandaa kumkabidhi rambi rambi mhanga bwana Massawe almaarufu Malanja
Katika harambee hiyo wanamichezo pamoja na wadau wote walionyesha kuguswa sana ajali hiyo ambapo kwa muda mfupi tu zilipatikana pesa taslimu zaidi ya shilingi laki nne na ahadi zaidi ya shilingi pia toka katika vilabu vilivyoshiriki harambee hiyo.
Mwenyekiti wa Kunduchi Kwanza Asia Mohamed akimkabidhi Malanja mchango wa harambee
Bwana Malanja akiwaonesha wadau mchango alioupokea
 Pia wadau walichangia vifaa ambapo klabu ya Kawe wao waliahidi kuchangia zaidi ya viunga mia moja vya makuti mara tu ujenzi utakapoanza pamoja na kutoa ushauri wa kitaalamu.  Mwakilishi wa Kunduchi Veterani pamoja na wanachama wao wote waliahidi kuchangia viti 10 katika harambee hiyo pia. 
Kunduchi Veterani
Jumla ya michango yote ilikuwa takriban shilingi milioni moja na laki mbili na nusu. Akizungumza baada ya kukabidhiwa mchango huo, bwana Malanja alitoa shukrani kwa wanamichezo wote walioshiriki katika harambee hiyo na pia alieleza namna alivyoguswa na upendo walioonyesha wana Kunduchi Kwanza tangu ilipotokea ajali hiyo ya moto mpaka sasa ambapo wamekuwa wakimpa moyo na kuahidi kutoa ushirikiano wao pindi ujenzi utakapoanza. 
Mzee risasi akiwa na Malanja

Mopao na mzee Ole
Akipokea shukrani hizo kwa niaba ya wanamichezo na wadau mweka hazina wa Namanga bwana Michael J Juma almaarufu Mopao alimhakikishia bwa Malanja kuwa kwa mchango huo wanamichezo wameonyesha ni jinsi gani wana upendo kwakwe na kumuomba aupokee kwa moyo mmoja kwa hicho ndicho wadau walichojaaliwa kukipata kwa wakati ule. 

Mdau akichagiza kwa dansi kuashiria kukamilika kwa harambee

Wadau wakiserebuka

Baada ya kumalizika kwa harambee, wanamichezo na wadau wengine waliendelea kupata burudani mbalimbali zilizokuwa zikitolewa. 
Baadhi ya wana Kunduchi Kwanza wakiongozwa na Katibu Msaidizi Bi Sizya Risasi (wa kwanza kulia)

Friday, March 08, 2013

JUMAPILI HII JOGGING NI KUNDUCHI KWANZA

Katika kuhamasisha uimarishaji wa afya kwa kutumia michezo pamoja na kuimarisha ujirani mwema klabu ya michezo ya Kunduchi Kwanza kwa kushirikiana na vilabu vya Namanga, Kawe na Biafra pamoja na wadau wengine iimeandaa na kuwaaliaka wadau wote katika mazoezi ya mbio za pole pole (jogging) ambazo zinatarajiwa kufanyika Jumapili tarehe 10 Machi, 2013 kuanzia saa 12:20 asubuhi. Ruti ya mbio hizo itaanzia katika makao makuu ya klabu ya Kunduchi Kwanza - Malanja Pub na kisha kuzunguka maeneo mbalimbali ya kata ya Kunduchi na hatimaye kumalizika hapo hapo Malanja Pub ambapo wanamichezo watapata fursa ya kujumuika pamoja na kujadiliana maswala mbalimbali yanayohusu mchezo wa mbio za pole pole.

MWALIKO WA KUSHIRIKI MAZOEZI JUMAPILI
Akizungumzia mazoezi hayo, Katibu Mkuu wa Kunduchi Kwanza Jogging alisema kuwa siku hiyo itakuwa ni maalum kwa wanamichezo kumpa pole mwanachama wa klabu ihoy ambaye pia ni mmiliki wa Malanja ambaye alipata ajali ya kuunguliwa na eneo lake la biashara. Hivyo hakutakuwa na michezo mingine zaidi ya jogging tu.Alieleza zaidi kuwa mbio hizo zinatarajiwa kuwa na urefu wa takriban kilomita 7.



Thursday, March 07, 2013

HARUSI, HARUSI, HARUSI!

Wanamichezo toka klabu za kunduchi Kwanza, Biafra, Namanga na vilabu vingine rafiki, wadau, wote, ndugu, jamaa na marafiki waungana pamoja katika kufanikisha harusi ya mwanamichezo toka klabu ya Namanga ndugu Jamal (zamani akijulikana kwa jiina la John) L. Gako ambaye anatarajia kufunga ndoa  mwishoni mwa mwezi Aprili mwaka huu. 

Bwana harusi mtarajiwa - Jamal L. Gako 


Bi Harusi Mtarajiwa wa kwanza kushoto
Katika kikao cha kwanza cha harusi hiyo kilichofanyika katika ukumbi wa Leecarz Pub Namanga na kuhudhuriwa na wanamichezo kutoka katika vilabu mbalimbali pamoja na wadau wengine, ulifanyika uteuzi wa uongozi wa kamati ya harusi hiyo ambapo Ndugu David Mwaka - Mwenyekiti, Abdul Mollel - M/Kiti Msaidizi, Andrew Mangole - Katibu, KP - Katibu Msaidizi, Michael Juma - Mweka Hazina. 

Wajumbe wakiwa kwenye kikao cha kwanza cha harusi
 Katika kikao hicho pamoja na mambo mengine iliamuliwa kwamba sherehe ya harusi hiyo itafanyika katika ukumbi wa bwalo la polisi Oyster-Bay Dar es Salaam. Vile vile iliamuliwa kuwa kikao cha pili kitafanyika katika ukumbi wa Leecarz namanga tarehe 10 Machi, 2013 kuanzia saa 11:00 jioni.

Wadau toka Namanga, Kunduchi na Biafra katika picha ya pamoja

Viongozi na wanachama wa Biafra Sports Club wanawatakia maharusi ndoa yenye baraka tele!!!

 



Tuesday, March 05, 2013

REQUEST FOR THE SPONSORSHIP OF BIAFRA YOUTH (U17) CUP 2013


Biafra Sports Club is organizing Biafra Cup (U17) Football competition which is scheduled to take place from the 2nd day of June to the 7th day of July. The tournament is expected to be strong and competitive one whereby 16 youth teams from various sports academies will participate in the tournament. 

Speaking about the tournament, the Secretary General of Club one Mr. yahya Poli informed that, The theme for the said competition is “IBUA NA ENDELEZA KIPAJI CHA KIJANA”. The 2013 Biafra Cup (U17) objectives are: -  
1. To provide young players and match officials with an opportunity to showcase their talent as well as  promote their physical and mental health and wellbeing, 
2. To assist young players to acquire and develop different football characteristics through contact with their peer,  
3. To mobilize young players and instill a sense of fair play in the best traditions of true sportsmanship,To raise awareness on the harmful social and cultural practices that are affecting children and youths at large such as drug abuse, HIV/AIDS and STDs, children’s rights through peer to peer discussion, distribution of leaflets and brochures, banners, e.t.c.
4. To promote and encourage other stakeholders to organize healthy, competitive recreation tournaments for young players. 
The tournament will take place during the month which the African continent and the world at large commemorate THE DAY OF AFRICAN CHILD on 16th June, 2013. The the for Day of African Child 2013 is "Eliminating Harmful Social and Cultural Practices Affecting the Children" therefore the organizing committee will use the tournament to raise awareness of children rights to commemorate  the said day.
 
The match officials from Twalipo Youth Soccer Foundation are expected to participate in the said tournament as referees and assistant referees in all 56 matches to be played. The said foundation train and provide refereeing skills to youths who are talented and interested to become referees in their future. These young referees have performed well in various youth tournaments such as Copa Coca Cola finals, Uhai Cup, NSSF Cup, e.t.c. to which they were participating as match officials.


He said further that, there will be various prizes to be awarded to the winners and other officials in different categories such as; the champion of the tournament, second winner, top scorer, the best disciplined player of the competition, best disciplined team of the competition, the best official, certificate of participation for each participating team and officials, e.t.c.

In order to meet the tournament’s outlined objective and budget successfully, facilitation as well as sponsorship is highly needed. Sponsors will play a very important role of facilitating the tournament by providing fund/grant and or facilities required for the tournament.

By sponsoring/facilitating the tournament sponsors on their part will have the opportunity to display and publicize their services or products during the matches and the tournament will be a platform whereby these sponsors will meet their customers/clients/communities especially youths, 


IBUA NA ENDELEZA KIPAJI CHA KIJANA 

CONTACT:
THE SECRETARY GENERAL,
BIAFRA SPORTS CLUB,
+255 715 253 6563
EMAIL: biafra.jsclub@gmail.com



Sunday, March 03, 2013

MAZOEZI YA MBIO ZA POLE POLE JUMAPILI TAR 3 MACHI YANOGA

Kama ilivyo ada, baada ya kuhairishwa ka safari ya kwenda kunduchi wanamichezo toka vilabu vya Namanga na Biafra waliamua kufanya mazoezi pamoja kwa kuanzia Namanga na na kuishia Biafra. Mbio hizo zilipita katika bara ya Ubalozi (USA), Old bagamoyo, Migombani, Mission Mikocheni, Mwai Kibaki, Mwinjuma, Hospitali ya Mwananyamala, Dunga, Kawawa na kuishia 90 Degrees Pub ambapo ni Makao makuu ya klabu y Biafra. 
Jogging barabara ya ubalozi (USA)


Katibu Mkuu wa Biafra akiongoza jahazi







Mara baada ya kumaliza jogging wanamichezo waliendelea na mazoezi ya aerobics yaliyokuwa yakiongozwa na mwanabiafra Khamis Suleiman (mwenye fulana nyekundu pichani chini).
 


Wanamichezo wote baada ya kutula walikaribishwa na Katibu Mkuu wa Biafra na baada ya pongezi za kushiriki na kumaliza mbio kwa wanamichezo wotw, taarifa mbalimbali zilitolewa ikiwemo ya  maendeleo ya mchakato wa kuanzisha Shirikisho la Jogging Manispaa ya Kinondoni pamoja na hatua zilizochukuliwa katika kuhuisha Chama cha Mchezo wa Jogging Kinondoni.
Katibu wa Biafra akiwakaribisha wanamichezo





Kutoka kushoto; Mary, Kaka Poli, na Bebee

 Safari yetu ya Kunduchi itafanyika jumapili ya tarehe 10 Machi, 2013. Karibuni wadau wote!!!

MAZOEZI NI AFYA ACHA KUJIACHIA!!!