Tuesday, December 06, 2011

HARAMBEE YA KUCHANGISHA FEDHA KWA AJILI YA KUFANIKISHA SHUGHULI YA KUFANYA USAFI NA KUTOA MISAADA KWA WAGONJWA KATIKA HOSPITALI YA MWANANYAMALA YAFANA SANA

Siku ya Jumapili, tarehe 4 Disemba, 2011 katika hafla ya uzinduzi wa Royal Billy's Lodge ambayo ipo nyuma ya Kanisa KKKT Tangi-Bovu palifanyika pia harambee kwa ajili ya kuchangia shughuli ya kufanya usafi wa mazingira katika Hospitali ya Mwananyamala pamoja na kutoa misaada ya hali na mali kwa wagonjwa katika wodi ya wazazi na wodi ya watoto hospitalini hapo. Kabla ya kuanza kwa hafla ya uzinduzi wa lodge hiyo na harambee, wakimbiaji wa mbio za pole pole (jogging) kutoka vilabu vya Biafra, Namanga, Kunduchi, Mbezi Beach, Temeke na wenyeji Tangi Bovu walikimbia mbio hizo kutoka Tangi Bovu kupitia Kawe na kurudi Tangi Bovu.
 Baada ya mbio za pole pole kumalizika wakimbiaji waliendelea kufanya mazoezi kwa mtindo wa aerobics na kama kawaida ili aerobics inoge basi unapigwa muziki na kaka Michael J almaarufu Mopao anaongoza mazoezi hayo

 Mmoja wa wakurugenzi wa Royal Billy's Lodge ndugu Tobias Owur akiingia wa mwisho baada mbio za pole pole - wakimbiaji wengi hawakumaliza mbio kwa kukimbi kama zilivyoanza.

 Wana-jogging wengine walifikia vitini kama anavyoonekana kaka Mustafa Muro

 Kutoka Kushoto ni Mama Kenisha Mkurugenzi wa Biafra Sports Club, Tobias Owur mmoja wa wakrugenzi wa Royal Billy's Lodge na Abdul A. Mollel Mwenyekiti wa Biafra Sports Club

 wana-jogging wengine waliona viatu ni vizito na havivaliki tena

 Dada Edita wa Namanga Jogging akinyoosha kiuno baada ya mbio

 Wakiwakilisha Biafra - Kutoka kushoto Jacqueline Mugalura, Yahya Poli na Ally Masharubu
 Mbusilo Joseph - katibu wa Kunduchi Kwanza pamoja na KP wa Temeke Jogging

 Noah Machaka wa Biafra

 Baada ya kumaliza mbio na burudani za hapa na pale, wana-jogging waliingia ukumbini kwa ajili ya kuanza harambee. Ndugu David Mwaka ambaye ni Mwenyekiti wa Namaga Jogging na Mkurugenzi wa Esoshi General Trading akiwakaribisha wageni ukumbini

 Katibu wa kamati ya maandalizi akiweka mambo ya teknolojia sawa sawa akiwa sambamba a mhamasishaji wa kamati toka klabu ya namanga Charles Juma

Mdau Henry Byarugaba akiingia ukumbini, yeye pamoja na mchango wa fedha ameongeza pakiti 100 za maziwa ya Tanga Fresh toka kwenye idadi ya awali ambayo 400 hivyo kufikisha idadi ya pakiti 500

 Mhamasishaji wa kamati Charles Juma alipigishwa magoti na kugombolewa ambapo pesa iliyopatikana iliongezewa kwenye mahitaji ya kukamilisha shughuli hiyo.

 Bwana Benson Simba akiwasilisha ahadi ya Royal Billy's Lodge na Dabenco Enterprises ambao wamechangia fedha taslimu pamoja na fulana kwa ajili kuvaliwa siku hiyo.

 Tobias Owur Almaarufu mkenya (mwenye miwani) akiwasilisha mchango wake

 Mama Kenisha akipiga makofi baada ya kuahidi kuchangia fedha tasilimu pamoja na katoni kadhaa za sabuni

 Mama Kenisha na Tobias Owur wakisoma ujumbe mfupi wa maandishi toka kwa wadau walio nje ya ukumbi ambao nao wameahidi kuchangia zoezi hilo

 Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi Abdul Mollel sehemu ya fedha zilizokusanywa papo hapo kwenye harambee

 Baada ya harambee kumalizika na Charles kugombolewa ilikuwa ni vicheko na furaha tele kama wanavyoonekana mama Kenisha, Mopao na Charles mwenyewe wakicheka kwa furaha

 Katibu wa kamati ya Maandalizi akiteta na wadau mbalimbali
 Meza iliwakilishwa na Mollel ndugu Joseph Mwaka (katikati) na Mjomba Ole

 Katika picha ya pamoja ni wana-jogging




Saturday, December 03, 2011

WADHAMINI WAJITOKEZA KWA KUJITOLEA MISAADA KATIKA HOSPITALI YA MWANANYAMALA TAREHE 9 DISEMBA, 2011

KATIKA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA A BIAFRA SPORTS CLUB, NAMANGA SPORTS CLUB PAMOJA NA KUNDUCHI KWANZA SPORTS CLUB AMBAO KWA KUSHIRIKIANA SIKU YA TAREHE 9 DISEMBA, 2011 AMBAYO NI KILELE CHA MAADHIMISHO YA KILELE CHA MIAKA HAMSINI YA UHURU WA TANZANIA BARA WATAFANYA USAFI WA MAZINGIRA NA KUTOA MSAADA KWA WAGONJWA KATIKA WODI YA WAZAZI NA WODI YA WATOTO KATIKA HOSPITALI YA MWANANYAMALA;

KAMPUNI YA ESOSHI GENERAL TRADING COMPANY LTD AMBAYO NI WAKALA WA KAMPUNI YA MAZIWA YA TANGA FRESH WAJITOLEA PAKETI MIA NNE (400) ZA MAZIWA YA TANGA FRESH  NA KAMPUNI YA TKT LTD YA DAR ES SALAAM WAJITOLEA CHUPA ZAIDI YA MIA TATU (300) ZA MAJI PAMOJA NA MIKATE NA BISKUTI.

MISAADA YOTE HIYO ITAGAWIWA KATIKA WODI YA WAZAZI PAMOJA NA WODI YA WATOTO HOSPITALI YA MWANANYAMALA DAR ES SALAAM SIKU YA TAREHE 9 DISEMBA, 2011.
 


MWANANCHI POPOTE ULIPO, KAMA UNAGUSWA NA KUUNGA MKONO BASI HUJACHELEWA KABISA, MSAADA WAKO WA HALI NA MALI UNAHITAJIKA. WASILIANA NA KATIBU WA KAMATI YA UFANIKISHAJI WA SHUGHULI HIYO KWA NAMBA 0715 253 653 AU KWA BARUA PEPE biafra.jsclub@gmail.com

Monday, November 28, 2011

KATIKA KUSHEREHEKE MIAKA 50 YA UHURU - BIAFRA SPORTS CLUB YAKUSUDIA KUFANYA USAFI WA MAZINGIRA NA KUTOA MISAADA KATIKA HOSPITALI YA MWANANYAMALA TAREHE 9 DISEMBA, 2011

BAADHI YA VIONGOZI WA KLABU ZA BIAFRA, NAMANGA NA KUNDUCHI KWANZA

Klabu ya michezo ya Biafra kwa kushirikiana na klabu za michezo za Namanga na Kunduchi Kwanza wanawakaribisha wanamichezo, wadau wa michezo na wananchi kwa ujumla katika zoezi la kufanya usafi wa mazingira pamoja na kutoa misaada katika hospitali ya Mwananyamala ambayo ni Hospitali ya wilaya ya Kinondoni.

Zoezi hilo la kufanya usafi na kutoa misaada katika hospitali hiyo ni katika kutimiza wajibu wetu kama jamii hasa katika kusherehekea miaka 50 ya uhuru wa Tanzani ambao kilele chake kitakuwa tarehe 9 Disemba, 2011. Kamati teule ya maandalizi ya shughuli hiyo inakaribisha maoni, mapendekezo, ushauri, michango na misaada kutoka kwa watu wote watakaoguswa na dhamira hii kwa kuwasiliana na Katibu wa Biafra Sports Club ndugu Yahya Poli: +255 715 253 653, au tuandikie barua pepe biafra.jsclub@gmail.com

Kauli mbiu ya sherehe za miaka 50 ya uhuru kwa mwaka huu 2011 ni TUMETHUBUTU, TUMEWEZA, TUNASONGA MBELE! MICHEZO NI AFYA, MICHEZO USHIRIKIANO, MICHEZO NI UMOJA! 

Wednesday, November 09, 2011

HAFLA YA SHUKRANI ILIYOANDALIWA NA BIAFRA SPORTS CLUB YAFANA SANA

Siku ya Ijumaa tarehe 4/11/2011 kulikuwa na hafla ya kupongezana ambayo iliandalia kwa pamoja na ya Biafra Sports Club  na 90 Degrees Pub Kinondoni. Kupongezana huko kulitokana na kukamilisha mchakato wa kuandaa/kuandika katiba ya Biafra Sports Club ambapo zoezi hilo lilifanyika kwa ushirikiano na msaada mkubwa sana wa mawazo na maoni toka kwa klabu rafiki za Namanga Jogging Club pamoja na Kunduchi kwanza Jogging Club.  

Wadau wakibadilishana mawazo wakiongozwa na Ally Masharubu mwenye kaptula

wageni toka Namanga Jogging na Kunduchi Kwanza Joggin walianza kuwasili ukumbini saa 12 jioni huku wanabiafra wakiwakaribisha kwa bashasha na majadiliano ya hapa na pale katika kuboresha klabu zetu za jogging
 
wadau wa Namanga na Biafra Jogging wakibalishana mawazo kabla ya kuingia ukumbini

Richie Richie mzee wa Riddy Sound "in the house" alitoa burudani ya nguvu kwa wadau waliohudhuria hafla hiyo ambapo alicheza nyimbo mbalimbali na kukonga nyoyo za watu wote ukumbini ambapo kila mara watu walisimama kucheza na kushangili kwa nguvu.
Richie Richie akiwazungusha wadau
Wadau wakiwa na furaha tele huku wakiburudishwa na muziki wa Richie Richie

ukawadia wakati muafaka wa kutoa shukrani kwa klabu rafiki za Namanga Jogging na Kunduchi Kwanza Jogging pamoja na wadau wote waliowezesha kukamilika kwa katiba ya Biafra Sport Club ambapo kwa niaba ya viongozi na wanachama wa Biafra Sports Club Katibu wa Biafra Sports CLub alizungumza machache ya kuwashukuru na pia alikabidhi bahasha zenye andiko rasmi la shukrani kwa viongozi wa Namanga Jogging na Kunduchi kwanza Jogging Club kama inavyookana kwenye picha hapo chini.
Makatibu paleeeeee Mbusilo Joseph (Kunduchi Kwanza Jogging) Kaka Poli (Biafra Sport Club)

Viongozi wa Namanga Jogging na Kunduchi Kwanza Jogging baada ya kukabidhiwa Bahasha

Katika kumalizia hafla na itifaki kadhaa, burudani na shangwe ziliendelea mpaka majogoo kama anavyoonekana Makamu mwenyekiti wa Biafra Jogging - Mollel aka Mutu hapo chini.
Makamu Mwenyekiti wa Biafra Sports Club (mwenye suti) Abdul Mollel

Wednesday, November 02, 2011

KARIBU UPATE BURUDANI YA RIDDY SOUND SIKU YA IJUMAA TAREHE 4/11/2011 NDANI YA 90 DEGREES PUB KINONDONI

RICHIE RICHIE - MZEE WA RIDDY SOUND IN THE HOUSE

Baada ya mchakato wa kuandika Katiba ya Biafra Sports kukamilika, wanachama wa Biafra Sports Club kwa kushirikiana na uongozi wa 90 Degrees Pub (ambapo ndipo makao makuu ya klabu) unayofuraha kuwaalika wananchi wote na wana-jogging toka klabu za Temeke, Kunduchi, Namanga, Makongo na kwingineko tujumuike pamoja na kupata burudani ya muziki mwanana toka katika bendi ya Riddy Sound chini ya uongozi wa Richie Richie (pichani juu). Burudani hiyo itaanza saa 1 kamili usiku na kuendelea. Karibuni tupongezane baada ya kazi ngumu na muhimu!!!!!!
ENEO LA TUKIO - 90 DEGREES PUB

WOOOOOOOOOOOOOOTE MNAKARIBISHWA

Saturday, October 29, 2011

BIAFRA JOGGING NA NAMANGA JOGGING NDANI YA TEMEKE

Robert Mwakibugi (mwenye tracksuit nyekundu) akiwakilisha Biafra Jogging

Emmi Msechu (mwenye usongo) akiwakilisha Biafra Jogging

Wadau wa Namanga Jogging

Timu ya ngumi ya Temeke Jogging

Mbio za pole katika barabara ya uhasibu - temeke

Baadhi ya viongozi wa Namanga Jogging wakito shukrani kwa wanatemeke jogging



Dada Mary - Katibu wa Namanga Jogging

BIAFRA JOGGING NA NAMANGA JOGGING NDANI YA TEMEKE

Dada Mtumwa wa Temeke Jogging akiongoza mbio za pole

Ibrahim Mpore aka King A.Y. Mpore (mwenye fulana ya bluu) akiwakilisha Biafra Jogging

Watoto nao hawakuachwa nyuma

Ally Masharubu (mwenye bukta nyeusi) akiwakilisha Biafra Jogging

Kutoka Kushoto Henry Maseko (Biafra Jogging), Charles (Namanga Jogging) A. Mollel (Biafra Jogging

Baadhi ya viongozi na wanachama wa Biafra Jogging wakitoa shukrani kwa Temeke jogging

Wednesday, October 19, 2011

KUNA UMUHIMU WA MATAYARISHO YA MWILI (WARM UP) KABLA YA KUANZA MAZOEZI

WANAJOGGING WAKIFANYA "WARM UP" KABLA YA KUANZA MBIO

"Warm Up" husaidia kuuweka mwili tayari kwa ajili ya mazoezi. Vilevile husaidia kuongeza kasi ya usambazaji wa damu katika viungo pamoja na misuli ya mwili pamoja na kuupa mwii joto kwa matayarisho ya mazoezi utakayofanya ambayo husaidia kulainisha viungo vyako vya mwili, hata hivyo husaidia kulainisha mishipa inayopeleka damu kwenye moyo na kusaidia kulinda misuli isipate madhara pamoja na mifupa.

pia, husaidia kuongezeka upatikanaji na usambazaji wa hewa ya oksijeni mwilini hasa kwenye misuli na mishipa ya fahamu.

TUWASHIRIKISHE WATOTO WETU KWENYE MAZOEZI

KAKA MOPAO AKIONGOZA KWARIDE LA WANAMAZOEZI